Ufunguo
JF-Expert Member
- Aug 18, 2012
- 330
- 231
Kwa wale mnaoratajia kununua Hiace kwa ajili ya kutoa huduma ya usafirishaji maeneo ambayo usafiri huu bado ni muhimu (hususani maeneo ya miji midogo na ama kusafirisha wanafunzi maeneo ya mijini) kuweni macho na TRA.
Jamaa yangu mmoja amenunua Hiace baada ya kuona katika Calculator ya TRA (Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools) kuwa Hiace zote ziko katika kundi la Utility ikiwa ni pamoja na magari mengine kama vile: Toyota Hilux, Canter, Nissan Hard body, Rosa, Coaster, Civilian, na kwamba magari yote katika kundi hili yana aina tatu tu za ushuru (kwa magari chini ya 2004) , yaani Import duty 25%,Excise duty 5%, na VAT 18%).
Baada ya Hiace kufika BANDARINI ndipo yakampata majanga.
· Wanamwambia kwakuwa Hiace yake ina viti vyote ndani sio utility
· Harmonised system (H.S ) code (Harmonized System - Wikipedia, the free encyclopedia) iliyopewa garin yake ni 87032399 (HS Code 87032399 | Harmonized System Code Other) badala ya H.S code 87029091 (Motor vehicles for the transport of ten or more persons, including the driver ITC HS CODE List.)
· Kwa mujibu wa TRA HIACE yake iko kwenye kundi la station wagon au racing cars (Station wagon - Wikipedia, the free encyclopedia, https://www.google.com.au/search?q=...7ICACA&sqi=2&ved=0CAcQ_AUoAQ&biw=1366&bih=667) .
· Kwa maana hiyo uwepo wa viti kwenye Hiace yake umeongeza kodi kutoka wastani wa milioni 5.5 hadi milioni 9 (karibu milioni 4!!).
· Kwa maana kwamba sasa atatakiwa kulipa aina nne za ushuru(yaani Import duty 25%, uchakavu 25% ,Excise duty 10%, na VAT 18%) tofauti na calculator inavyosema.
Ushauri:
· Ili kuondoa usumbufu kwa watanzania, na kuongeza uwazi kwa taasisi hii, TRA hawana budi kuorodhesha kwenye mtandao wao gari zote zinazotambulika kama "utility" nchini Tanzania ili wananchi waweze kujua na kujiandaa. Siyo lazima na ni usumbufu kama kila anayetaka kununua kitu nje ya nchi awasiliane kwanza na TRA kujua taratibu zinasemaje.
· TRA wanatakiwa kufanya marekebisho kwenye calculator yao (hususan eneo hili) maana linapotosha jamii badala ya kuelimisha
· Wale wanaotarajia kununua Hiace hakikisheni hazina viti ndani na/ama fanyeni utaratibu viti viondolewe hukokuko gari inapotoka au mara tu baada ya kufika bandari kavu. Hii ni kwa sababu marginal benefit ya Hiace isiyo na viti ni kubwa kuliko yenye viti.
TRA, HUU KAMA SIO WIZI NI UPOTOSHAJI MKUBWA