HOJA TRA watoe grace period kwenye ulipaji wa excise duty ya magarai

HOJA TRA watoe grace period kwenye ulipaji wa excise duty ya magarai

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

smtanzania

New Member
Joined
Jul 1, 2026
Posts
2
Reaction score
0
Baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha Bajeti ya mwaka 2026/27, Serikali imeongeza kodi ya excise duty kwa magari kulingana na uchakavu wake, ambapo ongezeko ni kati ya asilimia 5 hadi 10 kulingana na mwaka wa utengenezaji wa gari.

Sisi wafanyabiashara wa magari hatupingi kulipa kodi. Hata hivyo, tunaomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itoe kipindi cha mpito cha angalau mwezi mmoja kabla ya kuanza kutekeleza viwango vipya vya kodi. Wapo wafanyabiashara ambao tayari wana magari yako njiani au yaliyohifadhiwa kwenye bonded warehouses, hivyo utekelezaji wa ghafla unawaathiri kwa kiasi kikubwa.

Tunapendekeza TRA ifuate mfano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ambayo ilitoa kipindi cha mpito (grace period) wakati ilipofanya mabadiliko ya baadhi ya tozo. Hatua kama hiyo itawapa wafanyabiashara muda wa kujipanga na kupunguza athari za mabadiliko hayo.

Tunaomba uongozi wa juu wa TRA ulitazame suala hili na kuzingatia umuhimu wa kutoa kipindi cha mpito kabla ya kuanza kutekeleza viwango vipya vya kodi.
 
Back
Top Bottom