TRA wekeni mfumo wa wazi au App ya kuangalia taarifa za usajili na ulimiki wa Vyombo vya Moto ili kuepusha hizi kadi feki

polokwane

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2018
Posts
3,361
Reaction score
5,842
Napendekeza TRA waweke mfumo wa wazi ili watu waweze kutizama Taarifa za usajili wa gari, piki piki au bajaj ili kujia mmiliki halali ni nani

Mnaficha kitu gani kuweka mfumo huo kuwa huru? Mbona ni jambo ambalo linawezekana na ni jepesi tu

Hili litasaidia sana kuzuia watu kutengeneza kadi feki kwa sababu mtu akitaka kununua chombo cha moto anaingia kwanza kwenye mfumo nankutizama umiloko halali wa chombo hicho taarifa ambazo zitakuwa zimeunganishwa na NIDA na picha ya mmiliki.
 
Wizi wa siku hizi si kadi fake kwa jina fake bali ni kadi fake kwa duplicate ya kadi original. Hii itarahisisha kuongeza tatizo maana kama nina IST nyeupe ambayo ni ya wizi au haijasajiliwa nitakachofanya ni kuifahamu IST yoyote nyeupe, kuingia kwenye database na mm kutoa duplicate ya kadi na kuchongesha namba kisha kutafuta mjinga mjinga asiyefanya uchunguzi na kumuuzia wakamdake wakati anakata insurance.
 
Wanaficha kwakuwa wananufaika....upigaji nchi hii nikama sera
 
Wizi wa siku hizi si kadi fake kwa jina fake bali ni kadi fake kwa duplicate ya kadi original. Hii itarahisisha kuongeza tatizo maana kama nina IST nyeupe ambayo ni ya wizi au haijasajiliwa nitakachofanya ni kuifahamu IST yoyote nyeupe, kuingia kwenye database na mm kutoa duplicate ya kadi na kuchongesha namba kisha kutafuta mjinga mjinga asiyefanya uchunguzi na kumuuzia wakamdake wakati anakata insurance.
Unafikiri kwa ushauri wako njia gani itafaa kukabiliana na watu kuuziwa kadi feki?
 
Nikionana na mbunge wangu hapo baadae,nitamwambia apeleke kama swali la msingi kwenye "bonge" lijalo.
 
Kutoa taarifa za Wateja ovyo ni kinyume cha sheria. Upo utaratibu wa uhakiki wa chombo pale unapotaka kuuza/kununua ama kubadili umiliki kwa sababu yoyote ile.

Sheria ya usimamizi wa kodi sura ya 438, kipengele cha 3 Sehemu ya 21 kinaelezea vizuri suala hili.
 
Ipo njia kupata majina kadi ya Gari katika mfumo wa TRA, mfano ingia katika mitandao ya simu Kama unahitaji kukata Bima ya chombo, Kuna hatua utaona majina mmiliki chombo kabla hatua ya mwisho.
 
Unafikiri kwa ushauri wako njia gani itafaa kukabiliana na watu kuuziwa kadi feki?
Suluhisho ni mnunuzi kununua gari kutoka kwa mmiliki na sio dalali au mtu ambaye Jina lake halisomi kwenye kadi.

Hakikisha anayekuuzia gari ni mmiliki halali wa gari. Fata taratibu za manunuzi, chukua nyaraka zinazohitajika na badilisha kadi ndani ya muda husika.

OGOPA KAULI ZA SIKUBADILI JINA, MWENYE GARI YUPO MBALI, NINA MKATABA TU WA MAUZIANO ILA JINA SI LANGU. Hayo mambo kaa nayo mbali ikiwezekana unless mwakilishi ana nyaraka zote zinazohalalisha kumwakilisha muuzaji.

Tuache kununua gari kama viatu vya mtumba. Ukiachana na kutapeliwa pia kuna historia ya matumizi ya gari kihalifu n.k
 
Tatizo linakuja kumpata mmiliki anaye uza gari uitakayo ndio maana tunatumia madalali kwa sababu wai wanajua kutafuta magari kwa wauzaji , sasa mteja utajuaje kwamba gari ninayo itaka ni gx100 na mwenye nayo anaye uza ni bwana abdallah?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kutoa taarifa za Wateja ovyo ni kinyume cha sheria. Upo utaratibu wa uhakiki wa chombo pale unapotaka kuuza/kununua ama kubadili umiliki kwa sababu yoyote ile.

Sheria ya usimamizi wa kodi sura ya 438, kipengele cha 3 Sehemu ya 21 kinaelezea vizuri suala hili.
Hiyo ni miongoni mwa sheria za hovyo zilizo pitwa na wakati kwa ulimwengu wa sasa ,umiliki wa chombo sio jambo la siri wala la kuficha halina athari zozote kwa mteja, kama check namba zinabandikwa kwenye ubao wa matangazo hadi mama ntilie anazisoma sembuse taarifa za umiliki wa chombo?

Tanzania huwa tuko nyuma sana kuendana na wakati kwa mambo mengisana , bado tumekumbatia masheria ya kitumwa na kikoloni hadi sasa na hatutaki kubadilika ndio maana hadi sasa tunatumia katiba ya mwaka 1977 na sasa ni 2022
 
Tatizo linakuja kumpata mmiliki anaye uza gari uitakayo ndio maana tunatumia madalali kwa sababu wai wanajua kutafuta magari kwa wauzaji , sasa mteja utajuaje kwamba gari ninayo itaka ni gx100 na mwenye nayo anaye uza ni bwana abdallah?
Dalali si muuzaji wa gari ila ni daraja la mnunuzi kumfikia muuzaji wa gari. Dalali kazi yake ni kukufikisha kwa muuzaji wa gari, wewe kazi yako ni kuhakikisha muuzaji ni mmiliki halali na ana nyaraka zote zinazothibitisha hilo.
 
Wizi wa siku hizi si kadi fake kwa jina fake bali ni kadi fake kwa duplicate ya kadi original. Hii itarahisisha kuongeza tatizo maana kama nina IST nyeupe ambayo ni ya wizi au haijasajiliwa nitakachofanya ni kuifahamu IST yoyote nyeupe, kuingia kwenye database na mm kutoa duplicate ya kadi na kuchongesha namba kisha kutafuta mjinga mjinga asiyefanya uchunguzi na kumuuzia wakamdake wakati anakata insurance.
Sijui kama atakuelewa
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ipo njia kupata majina kadi ya Gari katika mfumo wa TRA, mfano ingia katika mitandao ya simu Kama unahitaji kukata Bima ya chombo, Kuna hatua utaona majina mmiliki chombo kabla hatua ya mwisho.

Tupe ujuzi mkuu,nikitaka niangalie sasa hivi umiliki wa chombo changu ni google wapi?
Toa maelekezo unafanyaje?
 
Napendekeza TRA waweke mfumo wa wazi ili watu waweze kutizama Taarifa za usajili wa gari, piki piki au bajaj ili kujia mmiliki halali ni nani

Mnaficha kitu gani kuweka mfumo huo kuwa huru? Mbona ni jambo ambalo linawezekana na ni jepesi tu

Hili litasaidia sana kuzuia watu kutengeneza kadi feki kwa sababu mtu akitaka kununua chombo cha moto anaingia kwanza kwenye mfumo nankutizama umiloko halali wa chombo hicho taarifa ambazo zitakuwa zimeunganishwa na NIDA na picha ya mmiliki.
Shida sisi watanzania ujanja ujanja mwingi maana hapo tu mmiliki hatumjui tunabumba kadi feki je na jina tukilijua sindiyo itakuwa hatari zaidi kubumba kadi? Ndiyo maana hata passport wanaficha baadhi ya taarifa ili ukibumba wakudake. Ushauri ni bora uwasiliane na tra wenyewe kama unataka nunua gari kujua kadi ni feki au.
 
Hata kwenye taarifa za mmiliki wanaweza kuficha baadhi ya identity kwa usalama lakini taarifa za awali kama jina na plate namba zikawepo
 
Unajua sisi wabongo tunajitengenezea wenyewe vizingiti.Ujanja ujanja unatuponza sana. Unauziwa kiwanja na kuna mtu mwingine kashauziwa hapo hapo hati hiyo imekopea benki na kiwanja chenyewe kipo kwenye eneo la hifadhi. Magari ndiyo usiseme unakuta wamekata chassis wanabandika namba ya gari kama hilo.Acha tu tupigwe pini maana forge zimezidi hatuoneani huruma mtu umehangaika kutafuta visenti angalau nawe uwe hata na IST yako unakumbana na jinga moja linakupigia fake. Na hapo kumbuka ndiyo kuna taarifa zimefichwa sasa ngoja zikiwa wazi sijui itakuwaje. kingine unanunu gari kumbe wewe ni mtu wa nne toka mmiliki wa kwanza kuliuza hapo chain nzima hawajabadili jina daaa
 
Back
Top Bottom