TRA yadaiwa kuanza kuvamia wawekezaji wa kigeni na kudai malipo na usuluhishi wa akaunti wa miaka 15 nyuma. Je, Serikali ina uhaba wa fedha?

Swala Walipe,kwani Ukikwepa Kodi ya miaka 20 nyuma ndio hudaiwi au inakuwa imetoka? Mzee jidanganye utafuatwa hata kama ni miaka 100
 
Hebu walipe kodi, mbona katika nchi zao wanalipa bila kulazimishwa, na huwa wanafukua historia ya ulipaji kodi ya miaka mingi nyuma
 
Kikubwa ni wao wavuke lengo la ukusanyaji, hawajui kesho watakosa hata sehemu ya kukusanya, unawezaje kuharass FDI wakati huna hata uwezo wa kuajiri 50% ya wahitimu wa vyuo ?

cc. TRA Tanzania
Ni ajabu Sana kaka, same time kuna uhaba wa dollar, halafu unaanza ku-frustrate hao wawekezaji wanaokuletea hizo $ kupitia FDI...... Nchi imejaa majizi yanafikiria kuiba na si kuboresha mazingira ya uwekezaji ili wawekezaji wawe wengi, ajira ziongezeke na serikali ikusanye mapato mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…