TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

Sababu zinazoleta matatizo haya ni mazingira ya kuzungumzia ulipaji kodi. Hakuna vikao halali vya kuzungumzia makadirio ya kodi. Wakusanyaji kodi wamegeuka kuwa Polisi. Hilo ndiyo tatizo kubwa. Kukusanya kodi huendi kumvamia mtu, au kumshtukiza. Na mnaposhindwa kukubaliana siyo upande mmoja ukachukue rungu la kuja kuua, huwa kuna takiwa kuwe na levels za majadiliano. Iko haja ya kuelewa maana halisi ya ulipaji kodi. Kwa taarifa tu wakwepa kodi bado wanaendelea, waliofungiwa wengi ni wazalendo wajasiria mali waliokataa kutoa hongo. Kwani si tunawajua wakusanyaji walivyo matajiri sasa hivi? Au mwingine anafanya hivyo ili kwa madhumuni apandishwe cheo tu. Tumeshasema hapa, biashara zote zilizokufa kwa sababu ya kodi zifanyiwe uchunguzi maalum na matokeo yawekwe wazi.
 
Hakuna mtu anayependa kuzaliwa bila kumjua baba/Mama yake, kama ulipata hiyo privilege mshukuru Mungu
Isiwe excuse ya kuwafanya wenzio matendo maovu kama aliyofanya Mwendazake. Ule unyama ni sawa na Iddi Amin tu
 
Ndiyo maana tumebaki kutembeza bakuli kwa wahisani ambao wakitupatia hiyo peanut wanakuja kuchukua raw material na madini yetu bure. Tunawaita eti wawekezaji. Yaani hayo madini na raw materials ni zao, waliziwekeza tu kwetu?
 
Hivyo dhana yakusema watu hawapendi kulipa kodi si sahihi.
Acha kudanganya. Duniani kote na enzi zote hakuna anayependa kulipa kodi. Vitabu vitakatifu kama Bibilia vimeandika hivyo. Mtoza ushuru alihesabika ni mdhambi ambaye akifariki moto wa milele ulikuwa unamngojea. Mtoza ushuru alihesabika ni agent wa shetani Lucifer. Ndiyo nature ya binadamu ilivyo. Lazima mabavu yatumike kukusanya hizo kodi. Mabavu hayo yamewekwa kwenye sheria za kila nchi. Ukitaka kuyaondoa basi ondoa au badilisha hizo sheria husika. Weka sheria za kubembelezana na majadiliano na miafaka ya kulipa au kutolipa kodi stahiki.
 
Ndugu ungekuwa unazielewa sheria za kodi basi ungekuwa umegundua yote uloandika hapo uko nje ya mada. Ndo maana kuna mtu alisema we need strong institutions and not strong people
Huyo mtu wako unayemsifia yuko wapi sasa
Elewa mada iliyo mezani vinginevyo utakuwa unademka tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…