TRA yakamata lita 1,240 za Ethanol na mifuko miwili ya sukari

TRA yakamata lita 1,240 za Ethanol na mifuko miwili ya sukari

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Kikosi cha FAST Bukoba kimefanikiwa kukamata madumu 62 ya Ethanol, yenye ujazo wa lita 20 kila moja, sawa na jumla ya lita 1,240 za Ethanol, pamoja na mifuko miwili ya sukari. Mizigo hiyo imekamatwa katika eneo la Bunazi, Wilaya ya Missenyi, Mkoani Kagera, ikiwa imeingizwa nchini kinyume na taratibu za forodha.

Kukamatwa kwa mzigo huo ni sehemu ya juhudi za TRA katika kudhibiti biashara ya magendo na kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingia nchini zinafuata taratibu na sheria za forodha.

TRA inaendelea kuimarisha operesheni na doria katika maeneo mbalimbali, hususan maeneo ya mipakani na njia zisizo rasmi, kwa lengo la kudhibiti magendo, kulinda mapato ya Serikali na kuhakikisha ushindani wa haki kwa wafanyabiashara wanaofuata sheria.

Ila watuuuu🙌🙌🙌🙌

MAFUTA 1.jpg
MAFUTA 2.jpg
MAFUTA 3.jpg
 
Back
Top Bottom