figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Wafanyabiasha wa Mafuta wa nje ya Nchi kutoka Congo, Malawi, Rwanda na Burundi wanalalamikia TRA kwa kuchelewesha Document kitu ambacho kinawatia hasara.
Tatizo hilo limeanza hivi karibuni. Ukipakia mzigo unaambiwa "System ipo down". Hali hii inafanya mfanyabiashara kusubiri Document siku 7 hadi 14 Wakati Mombasa Nchini Kenya Document unasubili saa mbili tu.
Mfano Watu wote waliopakia Petrol kwenye Kituo cha Oryx Bandari ya Dar es Salaam Tarehe 3 Juni 2024, hadi leo tarehe 11 Juni 2024 bado wapo Bandari wakisubiri Documents.
Sasa hivi Nchi ya Kenya imeongeza ufanisi. Zamani Document walikuwa wanasubiri Masaa sita kwenye Bandari ya Mombasa, ila sasa hivi ni Masaa mawili tu maximum.
MY TAKE
Bandarini na TRA kutakuwa kina watu wanafanya hujuma ili DP World ionekane si lolote si Chochote?
Nini kifanyike Tanzania tuondokane na tatizo hili?