TRA yatoa maelekezo ya Wafanyabiashara wa Mtandaoni kuonesha Vyeti vya Kodi

TRA yatoa maelekezo ya Wafanyabiashara wa Mtandaoni kuonesha Vyeti vya Kodi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
photo_2026-10-01_09-25-33.jpg
KUONESHA VYETI VYA KODI KWA WAFANYABIASHARA WANAOFANYABIASHARA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

Dar es Salaam 01 Oktoba, 2026

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawafahamisha wafanyabiashara na umma kwa ujumla kuwa mtu anayejihusisha na shughuli za kiuchumi zinazompatia kipato, ikiwemo biashara, ajira au uwekezaji, anatakiwa kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa mujibu wa Kifungu cha 22 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438.

Kwa kuzingatia marekebisho ya Kanuni ya 58 ya Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Jumla) za mwaka 2016, yaliyotangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 158G, mtu anayefanya biashara kupitia mitandao ya kijamii au majukwaa ya kidijitali anatakiwa kuonesha, kwa namna inayoonekana kwa urahisi kwenye akaunti au ukurasa anaotumia kufanya biashara, mojawapo ya vyeti vifuatavyo:

a) Cheti cha Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN); au

b) Cheti cha Uthibitisho wa Utekelezaji wa Wajibu wa kulipa Kodi (Tax ClearanceCertificate).

Kwa msaada na maelezo zaidi, tafadhali tembelea Ofisi za TRA zilizo karibu nawe au wasiliana na Kituo cha Huduma kwa wateja kinachopatikana kwa namba za kupiga bure 0800 750075 au 0800 780 078 au barua pepe [email protected].

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
Imetolewa na;
IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO
Screenshot 2026-10-01 094557.png
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mh hapa nafikiri kodi ya kichwa na maziwa kwa wanawake taratibu itarejea
 
Jamaa wanasaka pesa sana hivi miradi mikubwa Tanzania inapata kiasi gani mbona TRA mpo busy mpaka kwenye ishu ndogo ndogo kama vile Nchi haina kitu kama ipo Jangwani vile.
 
Zinazovuja na kuchezewa zingefidia mambo mengi.
Nchi yenu iko imejaa ******* ni wengi sana.
 
Jamaa wanasaka pesa sana hivi miradi mikubwa Tanzania inapata kiasi gani mbona TRA mpo busy mpaka kwenye ishu ndogo ndogo kama vile Nchi haina kitu kama ipo Jangwani vile.
Yusuph mwenda , anajipakulia mipesa kupitia team yake ya mpira
 
Yusuph mwenda , anajipakulia mipesa kupitia team yake ya mpira
Utadhani Nchi haina rasilimali yeyote ile utawaona wapo busy wanakimbizana na maboxi mtaani aisee Tanzania ina watu wana mawazo ya kimasikini sana aisee
 
Back
Top Bottom