TRAB na TRAT zasababisha TRA ikose kodi ya Tsh. Trilioni 2.8

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema TRA ilipanga kukusanya kodi ya Tsh. Trilioni 20.7 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021 lakini ilikusanya Trilioni 17.89 pekee.

Upungufu huo ambao ni 14% umetokana na kutoshughulikiwa ipasavyo kwa Madeni na Mashauri ya Kodi ambayo hayajatolewa uamuzi Mahakamani, Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) na Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT).

=====================

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Mamlaka ya Mapato (TRA) imeshindwa kukusanya kiasi cha Shilingi trilioni 2.8 kwa mwaka wa fedha 2020/21 kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kutoshughulikiwa kwa madeni na mashauri ya kikodi.

Akisoma taarifa ya Kamati hiyo bungeni Dodoma leo, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Japhet Hasunga amesema kuwa Mamlaka hiyo iliweka makadirio ya kukusanya kiasi cha Sh trilioni 20.7 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021 lakini kiasi halisi kilichokusanywa Tanzania Bara na Zanzibar kilikuwa ni Sh trilioni 17.89 pekee.

Nakisi hiyo ni sawa na asilimia 14 ya makusanyo hayo, ripoti hiyo imebainisha.

“Nakisi hiyo imechangiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutoshughulikiwa ipasavyo kwa madeni ya kodi pamoja na uwepo wa mashauri ya kodi ambayo hayajatolewa uamuzi katika vyombo vya Sheria kama Mahakama, Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) na Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT),” Bunge limeelezwa.

Kwa upande mwingine, eneo jingine ambalo taarifa ya Kamati imefafanua kwa kina ni malipo ya kiasi cha Dola za Marekani Milioni 153.43 yaliyofanywa na TANESCO kwa Kampuni ya Symbion kutokana na kuvunjwa kwa mkataba.

“Taarifa imebainisha kuwa, hasara hii ambayo Serikali imeingia inatokana na mapungufu katika makubaliano yaliyofikiwa kati ya TANESCO na Symbion pamoja na kutofanyika kwa upembuzi wa kina kabla ya kuvunjwa kwa mkataba huu,” amesema.

HABARI LEO
 
Court rulings siyo lazima iwe in favour of TRA. There is a big possibility that hizo kodi ni inflated or cooked up figures.
 
Hapo tupate mchanganuo ili tuweze kutenganisha, kiasi cha madeni yasiyokuwa mahakama/mashauri ya kikodi, nazile zilizopo mahakamani.

Uzembe mkubwa wa TRA ni kwa madeni yasiyokuwa ktk mashauri ya kimahakama.

Hayo yaliyopo mahakamani tuwatupie lawama zaidi hao TRAB na TRAT.
 
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema TRA ilipanga kukusanya kodi ya Tsh. Trilioni 20.7 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021 lakini ilikusanya Trilioni 17.89 pekee.

Upungufu huo ambao ni 14% umetokana na kutoshughulikiwa ipasavyo kwa Madeni na Mashauri ya Kodi ambayo hayajatolewa uamuzi Mahakamani, Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) na Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT).

=====================

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Mamlaka ya Mapato (TRA) imeshindwa kukusanya kiasi cha Shilingi trilioni 2.8 kwa mwaka wa fedha 2020/21 kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kutoshughulikiwa kwa madeni na mashauri ya kikodi.

Akisoma taarifa ya Kamati hiyo bungeni Dodoma leo, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Japhet Hasunga amesema kuwa Mamlaka hiyo iliweka makadirio ya kukusanya kiasi cha Sh trilioni 20.7 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021 lakini kiasi halisi kilichokusanywa Tanzania Bara na Zanzibar kilikuwa ni Sh trilioni 17.89 pekee.

Nakisi hiyo ni sawa na asilimia 14 ya makusanyo hayo, ripoti hiyo imebainisha.

“Nakisi hiyo imechangiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutoshughulikiwa ipasavyo kwa madeni ya kodi pamoja na uwepo wa mashauri ya kodi ambayo hayajatolewa uamuzi katika vyombo vya Sheria kama Mahakama, Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) na Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT),” Bunge limeelezwa.

Kwa upande mwingine, eneo jingine ambalo taarifa ya Kamati imefafanua kwa kina ni malipo ya kiasi cha Dola za Marekani Milioni 153.43 yaliyofanywa na TANESCO kwa Kampuni ya Symbion kutokana na kuvunjwa kwa mkataba.

“Taarifa imebainisha kuwa, hasara hii ambayo Serikali imeingia inatokana na mapungufu katika makubaliano yaliyofikiwa kati ya TANESCO na Symbion pamoja na kutofanyika kwa upembuzi wa kina kabla ya kuvunjwa kwa mkataba huu,” amesema.

HABARI LEO
Mbona Mwendazake asishughulikiw hizo Trab kwa mwaka woote 2020 kabla ya kuvuta kamba?

Mwigulu asisingiziwe hakuwa Waziri wa Fedha,Mpango yupo muulizeni.
 
Back
Top Bottom