Kiberege nina uzoefu nako. Ifakara sijawahi kufanya kazi kule. Swaraj zote zinazokuja kule ni 2wd, sijawahi kuiona ya 4wd. Kupata eka 40 hadi 50 kwa wiki inawezekana kama una dereva mzoefu wa maeneo ya kule au ukubali kufanya kazi na madalali. Bei ya juu ni elfu 45 kwa eka na bei ya chini ni 35 kwa eka(hii bei ya chini wanapenda sana watu wa swaraj kutokea kibaigwa na huwa wanakaa kijiwe cha peke yao maana wakichanganyika na wenye matrekta mengine hawapati kazi). Kama huwezi kusimamia mwenyewe hilo trekta nakuomba usilipeleke huko au usinunue kabisa hilo trekta. Narudia tena, kama huwezi kusimamia mwenyewe hilo trekta nakuomba usilipeleke huko au usinunue kabisa hilo trekta. Maana hutoiona pesa yake ila trekta utaona linachakaa tu. Kule kazi zipo nyingi tena ukiwa na trailer huwezi kukosa kazi. Ila ndo hivyo vizuri kula na wenzio, lazima upate mzoefu wa kule awe dereva wako au upate dalali. Kingine uwe mjanja, usiwe wa kukubali kila kitu. Fuatilia kila kitu wewe mwenyewe. Trekta likipata kazi ya kulima hakikisha upo hapo linapolima na wewe ndio uwe mpimaji wa ukubwa wa hilo shamba. Kila taarifa ihakiki na utunze kumbukumbu za hela zinazoingia na kutoka kupitia hilo trekta