Kizamani
JF-Expert Member
- Sep 12, 2011
- 418
- 108
Habari za jioni wana JF wenzangu na wapenda maendeleo wote kwa ujumla.
Ijumaa jioni, nikiwahi mjadala wa kufunga bajeti nilikamatwa kwa traffic. Nikiwa katika hali ya kuwahi kuangalia bajeti nikitokea Mwenge kuja ubungo, nilipita kwenye service road inayotokea sisimizi ambapo traffic waliokuwa wamejibanza walinikama. Nilikuwa sina jinsi ila kuwa chanzo cha mapato ya taifa letu, walifanya kazi yao.
Niliandikiwa buku 30 kwenye fomu ya "notification of traffic offences" na kwa sababu sikuwa na kiasi cha kutosha ilibidi nitafute Mpesa karibu, kilichonishngaza wakati wa kulipa niliona ile pesa inasokoteshwa kwenye origina ya ile fomu na mimi kupewa kopy yake. Ilibid nidai risiti ya serikali ambapo niliambiwa inabidi nisubiri yule traffic, ambaye nilisoma jina lake "Mwamakule", amalize kazi ndipo tuongozane mpaka ostabay polisi ndipo niandikiwe, nikala na matisho mengine mengine kwamba nikifika naweza kuwekwa ndani na mambo mengine aliyoongea, nikaona isiwe so, nikala kona.
Ishu yangu:
Je hii fomu ya traffic offences ni sawa na risiti halali ya serikali. Inafanyiwa oditing? je ni haki yangu kupewa risiti pale au kuzungushwa. Ni lazima kuwa makini kwani unaweza kuta buku 30 yangu either ilinywewa laga au kusuuzia rungu. Naomba mnielimishe nyie wenye experince na haya mambo ya traffic, sio kwamba nawalaumu kwa kufanya kazi yao.
Mwito wangu kwa wapenda maendeleo:
1. Ujue haki yako. Sio tu uende kwa mjumbe uambiwe leta buku kumi ili uandikiwe barua na wewe utoe tu, jua bia ya srikali ni shilingi ngapi.
2. Mnaonaje wana CDM wenzangu kwamba tutakavochukua nchi 2015 tuwashauri traffic na watumishi wengine wa serikali kwamba kama anaenda sehemu ambayo anajua atapokea malipo kwa naiaba ya serikali ni vema akwa na kitabu cha risiti halali ya serikali. Hii itasaidia kuondoa mianya ya kupoteza mapato ya serikali.
3. Nakushauri wewe unayesoma hii thread ingia CDM kwani utajifunza mengi. Mimi ni kama mwezi tu nimejiunga CDM na kuweza kuhudhuria vikao na wanachama wengine na nikajifunza mengi sana.