Traffic police na kosa la ubovu wa gari

Traffic police na kosa la ubovu wa gari

Hardman

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2011
Posts
748
Reaction score
524
Habari,
Juzi kuna mdau kasimamishwa na Traffic police anataka amwandikie fine kisa ubovu wa gari yaani bumper la mbele limeharibika,

Tulikua tunawaza, huu ujasiri wanautoa wapi? Bumper la gari limeharibika kutokana na ubovu wa barabara, kwa nini fine wasitozwe wajenzi wa barabara kwani wao ndo chanzo kikuu cha msingi cha ubovu wa gari( bumper)?

Ni mawazo tu, wadau mnaonaje?

Uzi tayari.
 
Bumper linahusiana vipi na usalama barabarani? Muongozo wa makosa barabarani ambayo trafiki wanapaswa kuyasimamia ni yapi?Je hilo ni mojawapo? Ukizungumzia ubovu wa gari unaangalia vitu gani?Hiyo siyo sahihi.!!!
 
Tuombe mwongozo "ubovu wa gari" ni kosa lipi hasa?
Traffic hili kosa wanalitumia visivyo.
 
ivi Bumper ndo linakaa/wekwa wapi kwa gari 🤣
 
Habari,
Juzi kuna mdau kasimamishwa na Traffic police anataka amwandikie fine kisa ubovu wa gari yaani bumper la mbele limeharibika,

Tulikua tunawaza, huu ujasiri wanautoa wapi? Bumper la gari limeharibika kutokana na ubovu wa barabara, kwa nini fine wasitozwe wajenzi wa barabara kwani wao ndo chanzo kikuu cha msingi cha ubovu wa gari( bumper)?

Ni mawazo tu, wadau mnaonaje?

Uzi tayari.
Zinatafutwa pesa kuna mfumuko wa bei hadi za kubrashia viatu juu
 
Tuombe mwongozo "ubovu wa gari" ni kosa lipi hasa?
Traffic hili kosa wanalitumia visivyo.
Niliisha wahi kumuachia leseni Trafiki eneo la Visiga(jina namhifadhi) kisa packing light nyuma, kushoto haiwaki Saa saba mchana na uzuri leseni ndiyo ilikuwa inaisha muda wake ( niliisha renew na ile sijaifuatilia hadi leo!)
 
daa ulimaliza kiume,kwo leo kaweka kwenye wallet yake akijinadi kuwa naye ana leseni!!
 
Niliisha wahi kumuachia leseni Trafiki eneo la Visiga(jina namhifadhi) kisa packing light nyuma, kushoto haiwaki Saa saba mchana na uzuri leseni ndiyo ilikuwa inaisha muda wake ( niliisha renew na ile sijaifuatilia hadi leo!)
Hilo nimelitatua kwa kutembea na bulb ya akiba,ikitokea tu haiwaki na wamenifumania,nawaonyesha bulb kuwa naenda kuifix
 
Kwahiyo kwa kosa la balbu kutokuwaka ndiyo uandikiwe gari bovu?
 
Back
Top Bottom