Traffic Police wa Tanzania wanasababisha ajali kuliko kupunguza

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Huu ndio ukweli mchungu sana.... Unamiliki chombo Cha usafiri? Wewe ni Mtu makini wakati wa Safari? Basi utakubaliana na ukweli huu.

1. Traffic Police wetu wamegeuka wakusanya mapato badala ya Usalama kwanza imegeuka Mapato kwanza. Ndio maana hushangai kusikia taarifa ya Jeshi la Police kujivuna kukusanya Kiasi kikubwa Cha fedha as if ndio their prime task.

2. Wanachangia kupunguza concentration barabarani, yaani badala ya kuendesha kwa kufuata sheria, unaendesha huku unamtafuta ni wapi Traffic Police amejificha...ghafla anajitokeza kutoka kusikojulikana.......Hali hii huweza kusababisha ajali endapo dereva Hana utulivu.

3. Ukaguzi fake wa magari unaofanywa na Askari hawa, ukweli mchungu ni kwamba Tanza-nia hatuna au tunao Vehicle Inspectors Wachache sana. Nenda pale Mbezi au Singida Bus stands ukute jamaa eti wanakagua bus 🚌 utaishia kucheka tu, jamaa anainama mvunguni sekunde anatoka anaruhusu basi.

4. Ukaguzi usiozingatia maeneo salama, yaani wakijisikia tu siku hio watasimama popote na kuanza kusimamisha, nakumbuka tulikoswakoswa ajali maeneo ya kati ya Mlandizi na Visiga pale, unakuta Askari kasimama katikati ya barabara, yaani ana amini kwakua yeye ni Askari basi automatic gari itamkwepa.....

5. Askari wamekithiri kwa rushwa, na hii Iko Kila Mahali, kama huamini sasa hivi ninavyoandika hivi tafuta Dereva wa kirikuu atakwambia kwanini inaitwa "wali Nyama" ni Kwa sababu wanatoa buku Hadi buku mbili kwa traffic.... asubuhi kapande basi za Mkoani Hadi Chalinze ukae siti ya mbele uone jinsi wanavyotoa nyekundu nyekundu, na siku hizi Wana ujanja wakiwasimamisha Askari Mmoja a apanda kwenye gari anawazuga huku Kondakta akimpa rushwa Askari mwingine ambaye Yuko chini.

6. Hakuna Askari awe IGP au Koplo asijeyajua mambo haya kuwa mabasi mengi ni mabovu sana sana, tunafika salama tu kwakua MUNGU anatupenda.

Ushauri wangu.

1. Askari wasilipishe faini, kuwe na chombo kingine, Mimi ni mdau wa kwanza miaka ile kushauri matumizi ya EFD kwa Askari Ila naona sasa Kuna haja ya kuboresha.

2. Stickers za usalama wa barabarani ni useless maana zinauzwa buku Tano pale Oyster bay na kwingine na hakuna ukaguzi unaofanywa kama mantiki ya sticker inavyokutaka.

3. Kuwepo na sehemu maalum za ukaguzi wa magari hasa highway na sio Kila pori tu.

Mtakuja kufa
 
asante kwa taarifa.
ila kiukweli trafik ni kero.
hata mkanda umesahau kuvaa anataka 5000.ovles kbs
 
😀😀😀tena
 
Hao askari wakitolewa barabarani miye naomba wananchi wanaoishi karibu na barabara wajichukulie sheria mkononi hata mawe waweke barabarani. Maana wakikaa kimya watagongwa kila siku na madereva vichaa.
 
Subutuuuuu yako
 
Ukitoa 10,000 kulipia sticker za usalama barabarani haurudishiwi chenji, sasa ulogwe uidai hiyo chenji uone kitakachofuata.
 
Zifungwe camera za barabarani sehemu zenye makazi ya watu
Hao askari wakitolewa barabarani miye naomba wananchi wanaoishi karibu na barabara wajichukulie sheria mkononi hata mawe waweke barabarani. Maana wakikaa kimya watagongwa kila siku na madereva vichaa.
 
Basi ndiyo trafiki washapunguzwa barabarani acha tuone, kati ya madereva walevi na trafiki wala rushwa nani ataibuka mshindi.
 
Back
Top Bottom