Traffic wanabambikia watu faini, unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na gari halijaenda popote

Traffic wanabambikia watu faini, unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na gari halijaenda popote

Inawezekana ulikutwa na kosa siku tatu au saba nyuma,askari hakuwa na mashine,inampasa afike kituoni kuwasilisha data muhimu kwa waliopigwa fine.
Utaratibu ni kwamba askari anaepokea hizo data alitakiwa akupigie simu kwanza kukufahamisha kuwa anakulima fine kwa kosa ulilofanya tarehe fulani mahali fulani
Lakini pia unaweza kuangalia kwenye mtandao aina ya kosa,lilitendeka wapi na tarehe ngapi utajua tu kama gari alikuwa nalo dereva au mkeo kwa siku hiyo
Asante Bro. Kabombe lakini katika siku tajwa mimi na mke wangu tulikuwa wote nyumbani na gari haikutoka siku nzima
 
Hapa ni rahisi.

Kwakuwa huwa wanaandika namba ya gari na leseni, waambie wakupe jina la mwenye leseni nae aitwe.
Unaongea kama mbuzi aliyetoka kupandwa muda si mrefu.

Unadhani hapa ni Ulaya.

Tena akichelewa kulipa baada ya wiki hiyo pesa ina Riba kubwa 🤣🤣🤣🤣
 
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.

Ukiingia kwenye mtandao wao wa tms.tpf.go.tz unasachi gari yako unaona kweli umeandikiwa kosa kwa muda huo lakini unakuta kosa hilo limefanyikia mkoani. Ukienda kuripoti tatizo hilo unaelekezwa uende traffic Central ili tatizo lako liweze kushughulikiwa na kitengo kinachohusika na malalamiko kama hayo.

Hapo sasa unaanza kuzungushwa kwani unaambiwa uache namba ya simu watalishughulikia na wanakueleza uwapigie kuwakumbushia. Sasa ukishaondoka hapo baada ya siku chache ukimpigia yule mhusika hapokei tena simu yako na ukitazama kwenye mtandao deni liko palepale.

Tunaomba wakuu wanaohusika ndani ya Jeshi letu la Polisi walitazame jambo hili la kubambikiwa faini kwani linawanyima raha wananchi wanaotumia vyombo hivi na kuwafanya wakose imani na jeshi lao la polisi ambalo tunaamini kuna maeneo wanafanya kazi vizuri sana.
Unaweza ukawa nyumbani kumbe dogo (mwanao) kachukua kaenda nalo sehemu wewe uko ubize mnaangalia VPL
 
Karibu Tanzania ya VIWONDER.
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.

Ukiingia kwenye mtandao wao wa tms.tpf.go.tz unasachi gari yako unaona kweli umeandikiwa kosa kwa muda huo lakini unakuta kosa hilo limefanyikia mkoani. Ukienda kuripoti tatizo hilo unaelekezwa uende traffic Central ili tatizo lako liweze kushughulikiwa na kitengo kinachohusika na malalamiko kama hayo.

Hapo sasa unaanza kuzungushwa kwani unaambiwa uache namba ya simu watalishughulikia na wanakueleza uwapigie kuwakumbushia. Sasa ukishaondoka hapo baada ya siku chache ukimpigia yule mhusika hapokei tena simu yako na ukitazama kwenye mtandao deni liko palepale.

Tunaomba wakuu wanaohusika ndani ya Jeshi letu la Polisi walitazame jambo hili la kubambikiwa faini kwani linawanyima raha wananchi wanaotumia vyombo hivi na kuwafanya wakose imani na jeshi lao la polisi ambalo tunaamini kuna maeneo wanafanya kazi vizuri sana.
 
Hao jamaa wa usalama barabarani(japo siku hizi ni faini barabarani) wamenifanya nidharau kazi yao, majitu hayajielewi, yanatumia nguvu nyingi akili kidogo.
 
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.

Hao ni jamaa zako, inakuwaje wabahatishe namba yako ya simu ikaendane na namba za gari lako?
 
Ilimkuta mzee wangu Arusha,leseni yake ina makosa 3 pamoja na aliyoshikiwa,mawili alipigiwa singida gari ikiwa ni Scania hajawahi endesha Scania maisha yake yote.Nadhani kuna michezo trafiki wanafanya au wakati wanaingiza namba ya leseni wanachanganya
 
Mbona simple tu, usilipe sometimea huwa wanakosea kwenye kuandika pale kwenye mashine mwisho wa siku huwa wanalipishana wenyewe...
 
yaani nilicheka juzi trafik kanismamisha katika kulumbana na kuelekezana maana tulikuwa kama wa3 na kosa ni kutotii zebra cross!!yule askari mwanamama ukidondosha ela kwenye kibanda chao pale chini hapohapo anajaza kiasi ktk simu yake.sbb nilikuw karibu pale niliona sim yke ilivyojaa mahesabu ya siku hiyo.siku ingine tena walinipiga toch nikaenda kwenye gar yao wakataka elf10 nikapiga saund hd efu5 akafungua ile glog box pale aweke ile elf5 ela zikamwagika chini mwenzake akawa anamfokea si unaona sasa ameona..
 
the bottom line hawa polisi trafik hawapo kivileee kusimamia hizo sheria maana hata wao sheria wengi wao hawazijui.mfano mmoja aliulizwa maana ya mistari 2 kati kati ya barabara hajui inachomaanisha yaani hadi aibu!ukute ndo mnabishania sasa kuhusu sheria anajifanya anajua huku hajui kikubwa atachokufanyia ni kutumia mamlaka yke kukunyanyasa!ndo mana wanalogwa sana.ila trafik wengine smart sana yaani umefanya kosa afu ukakubali anakuonya tuu safari inaendelea.yaani sasa hivi trafik wamekuwa wengi mabarabarani hadi ukiwa na mgeni huku tanzania anashangaa.huendi mita10 bila kuwaona trafik.trafik wengine mjirekebishe tutaanza kutembea na vikamera vidogo tuwarekod wakubwa wenu waone ufedhuli mnaofanya.
 
Hao ni jamaa zako, inakuwaje wabahatishe namba yako ya simu ikaendane na namba za gari lako?
Nadhani hujaelewa somo.Wakishachukua namba ya gari ni rahisi kumtafuta mwenye gari.
Ilimkuta mzee wangu Arusha,leseni yake ina makosa 3 pamoja na aliyoshikiwa,mawili alipigiwa singida gari ikiwa ni Scania hajawahi endesha Scania maisha yake yote.Nadhani kuna michezo trafiki wanafanya au wakati wanaingiza namba ya leseni wanachanganya
Mbona simple tu, usilipe sometimea huwa wanakosea kwenye kuandika pale kwenye mashine mwisho wa siku huwa wanalipishana wenyewe...
Walipishane wenyewe lakini basi kwenye system isionekane tena kama ninadiwa.
 
Nadhani hujaelewa somo.Wakishachukua namba ya gari ni rahisi kumtafuta mwenye gari.

Walipishane wenyewe lakini basi kwenye system isionekane tena kama ninadiwa.

Kwenye huo mfumo waondoe option ya kuona namba za simu badala yake kama kuna ulazima basi namba ya simu ikasome TRA tu
 
Kipindi hiki cha JPM hayo mambo wanayaogopa kama ukoma, kama yupo anaebandikiza watu makosa mripoti atumbuliwe chapchap.

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Hawa polisi JPM Keshabariki maovu yao. Hata useme vipi hawachukuliwi hatua yoyote. My take jihadhari na polisi vitengo vyote kadiri unavyoweza, epuka sana kutumia private means of transport. Zile POS walizopewa ni majanga unabambikwa kosa ukilalamika unaambiwa wamepewa malengo ya makusanyo. Ukiuliza mbona hiyo kazi ya kukisanya mapato siyo ya polisi ni ya Tra unaambiwa twende kituoni ukaseme hayo matusi mbele ya OCD. ukifika huko unawekwa ndani. Chezea polisi ya magu wewe!
 
Back
Top Bottom