Trafiki: Abiria wa Makumbusho-Posta wastaarabu siyo kama wale wa ruti ya Mbagala

Trafiki: Abiria wa Makumbusho-Posta wastaarabu siyo kama wale wa ruti ya Mbagala

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
FWUxJgCXwAEWCSJ.jpg
"Utakuta watu wa route hii ya Makumbusho Posta wana ustaarabu, akikuta gari limejaa kwanza hapandi, tofauti na route za Mbagala, hata mwonekano wa kondakta na dereva wa gari la Posta uko smart, "- Sgt Amin Iddi, Traffic Dar.

"Umepanda pikipiki dereva anaenda isivyo wewe unashindwa kumwambia?, kwa maana hiyo na wewe unakubaliana naye, hivyo jamii ichukue hatua katika hili hivyo tutasogea (kuepusha ajali)"- Sgt Amin Iddi, Traffic Dar es Salaam.

"Mtazamo wa wengi ni kwamba usafiri wa haraka ni bodaboda, abiria yeye ndiye anayemsukuma mwendeshaji amuwahishe anakokwenda, hapo unapata picha kwamba jamii na yenyewe inachangia,"- Sgt Amin Iddi, Traffic, Dar es Salaam.


Source: East Africa Radio
 
Hakuna ustaarabu wowote, ni hali ya usafiri tu.

Tofauti iliyopo Mbagala abiria ni wengi magari machache, lazima yagombaniwe.

Lakini kwa Makumbusho - Posta usafiri upo wa uhakika, hakuna sababu ya abiria kugombania basi.

Nakubaliana nae kwa upande wa bodaboda, abiria anapelekwa kwa mwendo kasi lakini yupo kimya tu, haongei lolote, ajali ikitokea "ni mapenzi ya Mungu."
 
anacho kisema kamanda 'Sgt Amin Iddi' ni kweli kabisa, yaani kuna maeneo ukiishii tegemea kabisa kuharibikiwa kifamilia au hata kimaisha etc.
 
Huyo askari ndio wale walioishia VII sasa ameshindwa kutumia akili ndogo kutambua Population ya watu waliopo Mbagala na idadi ya magari..? Hata kwa macho ukikaa stendi unaona idadi ya watu na magari ni tofaut kabisa.
 
Hata abiria wa mbagala akihamia ruti ya Makumbusho Posta au Ubungo Masaki lazima awe mstaarabu coz kuna abiria wachache.
Nenda hata SIMU 200 hapo uone abiria wa Tabata Kimanga au Mbezi wanavyodandia gari kikamanda.
 
Huyo askari ndio wale walioishia VII sasa ameshindwa kutumia akili ndogo kutambua Population ya watu waliopo Mbagala na idadi ya magari..? Hata kwa macho ukikaa stendi unaona idadi ya watu na magari ni tofaut kabisa.
ndio nyinyi mpaka upungufu wa nguvu za kiume mnahusisha na shule.

unapajua makumbusho au unapasikia jf???tena gari za hapa ni zile ndogo coaster sio gari kubwa tata.
 
Ngoja niifanye hii mada iwe more controversial, wakazi wengi wa makumbusho na maeneo jirani ni middle class,well educated na wengi wana private cars!,mbagala wengi ni mapokeo ya UPE na mchanganyiko wa Kayumba!!
 
Back
Top Bottom