Transformer la umeme mtaa wa Livingstone na Lindi lageuka kitega uchumi kwa wafanyakazi wa TANESCO

Transformer la umeme mtaa wa Livingstone na Lindi lageuka kitega uchumi kwa wafanyakazi wa TANESCO

Kuna Transformer ipo huku Tabora nayo ina tabia ya kukata fuse, mara Arrestor yaan shida tupu. Ukiwapigia simu wanakuja baada ya wiki moja. Ikawa ndo mchezo wao, sasa mimi nna biashara ya mashine eneo hilo so mi ndo nikawa naumia zaidi umeme ukikaa wiki haupo. Siku moja ikaunguza Arrestor wakaja baada ya siku 8 wakanambia niwe nawapa hela ili wawe wanawahi kuja kukarabati nikawajibu sawa. Nmeamua kununua mashine inayotumia mafuta ya Diesel umeme hata ukikata wiki sawa tu. Linchi la hovyo sana hili kilasiku najuta kuzaliwa Tz.
Si ungewapa hela yenye shoti ya umeme kutoka serikalini ili iwe fundisho kwao?
 
Hii nchi kuna mambo ya kishenzi sanaaa,,plz doto biteko najua uko umu acha kuchekacheka na washenzii,,anaezingua mweke pembeni weka mwingne

Vijana wamejaa tele mtaan mnalambanalambana uko kwa mambo ya kishenzi
 
Si ungewapa hela yenye shoti ya umeme kutoka serikalini ili iwe fundisho kwao?
Mkuu serekalini tunalindana uliza wote waliokamatishwa Ela za TAKUKURU kama wanafungwa wote ni kesi utasumbuana nayo miaka 2 after hapo unashinda unalipwa pesa zako unarudi kazini
 
.
255769421630_status_2bff4ea6d725410196ffad7f5e2ea64a.jpg
 
Mkuu serekalini tunalindana uliza wote waliokamatishwa Ela za TAKUKURU kama wanafungwa wote ni kesi utasumbuana nayo miaka 2 after hapo unashinda unalipwa pesa zako unarudi kazini
Wewe unamkamatisha tu. Hayo ya kuja kuachiwa huko mbeleni ni juu yao. Muhimu ni kwamba mpokea rushwa atakuwa amepata somo.
 
Hilo transformer kila siku TANESCO wanapigiwa simu, wakija wanataka pesa kulitengeneza fuse yake, wanaitegesha tegesha kihuni huni tu ili ifanye kazi kidogo, ikifika kesho yake inazima tena, ukiwapigia simu wanakuja ila wewe uliyewapigia inabidi uwape pesa watengeneze, wanachokonoa chokonoa fuse inafanya kazi, kesho inazima tena.., mchezo ndio huo kila siku.

Jana wamepewa pesa wakatengeneza, leo asubuhi likazima tena, toka asubuhi watu wamegoma kupiga simu, hakuna anaetaka tena kutoa pesa yake. Imagine Kariakoo hii panakosa umeme kila siku, watu wanaingia hasara ya mamilioni kwa sababu ya fuse, kweli?!!
Draft barua kwenda meneja wa Tabesco - Dar. Then itume kwa Whatsapp katika format ya PDF 0758 346 869.
 
Draft barua kwenda meneja wa Tabesco - Dar. Then itume kwa Whatsapp katika format ya PDF 0758 346 869.
Barua yangu nduo hii, sina nyingine, aione na arudishe umeme mtaa wa Lindi na Livingstone, hatuna umeme hadi sasa kila siku!!!
 
Yaani hii hali ni kila siku, tumeshatoa pesa hadi tumechoka, sasa hali hii hadi lini, magenerator yanatutia hasara, mafuta bei juu!!! Sasa hii manake nini??!!!
Kwa nini mtoe pesa? Kwa nini msiende kwa Regional manager mkamueleze mkiwa na references za mawasiliano mliyofanya kwa watu wake?

Huoni kama kuita watu na kuwapa hela ni kuchochea tabia rushwa bila sababu yoyote?
 
Usipotoa pesa wanakwambia tumeagiza kifaa, kinakuja lini hawasemi
 
Back
Top Bottom