Travelholic (wanaopenda kusafiri) na adventurers tukutane hapa

Travelholic (wanaopenda kusafiri) na adventurers tukutane hapa

Hata mm kusafiri ni hobby yangu ila tatizo vyuma vimekaza


Wenzetu walio endelea huwa wanatembea sana embu jiulize huwa wanatafuta nn..?

Asikwambie mtu kusafiri raha sana hasa unapo safari na bby mama wako aisee mnaenjoy sana




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikir mim pia ni Travelholic juz kat disemba nimepiga route ambayo nafikir sitasafir for four months yan sina ham! Nlitoka Dar to kigoma via dom, manyoni tabora then kasulu nikala pozi mjin kasulu then nikaanza kuitafuta mwanza kupitia kakonko, kibondo, nyakanazi, geita then mwanza duh nilichoka sana. Ila safar yang ya kwanza zanzibar na flying horse sitakuja isahau aiseee dakika 20 baada ya kutoka ferry nilitaman nimtafute mhudum ninwambie nirudisheni ferry [emoji28], tulitumia masaa matatu, picha linaanza engine moja ikazima wakapambana ikawaka kufika mbele mawimbi hatar, boti inayumba hakuna mfano, nikamuuliza mama mmoja hii hali ni kila siku?! Akasema 'hapana hata mim leo nashangaa'! Nilichofanya nikatuma msg kwa watu wangu wa karibu nikajikabidh kwa Mungu baba [emoji28]! Ila tulifika salama tukala bata sanaa!! At the mid of bata nikikumbuka kuna kurud bara nachoka [emoji28], kuna mtu akanambia panda Azam sea link ile ya mizigo you will feel nothing kweli bana nili enjoi kupanda lile dude tulitoka zanzibar sa nne usiku tulifika fery sa 11 alfajir! So far nimepita/tembea mikoa isiyopungua 15 (mikoa yote niliyokua nataman kutembelea nishaitembelea)! Najifunza vingi kupitia kusafir
 
Mbugani mzee huwaga kuna upekee wake sana...unapata aman ya moyo ya kweli. Ndy maana wazungu husafiri na kuja kukaa Serengeti hata mwezi mzima akitafakari maisha.
Safari yangu ambayo sitaisahau nilitembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire,asee ile kitu ni safi sana,huduma za tour guides ni nzuri sana,pia katika mzunguko wote nikamalizia na lodge yao inatwa Sopa (Sopa lodge),ile kitu ni hatari sana,iko katikakati ya mbuga,lakini huduma zote zipo.Sikuweza kuamini kuwepo kitu kizuri kama kile.Ni kweli unaposafiri ubongo unaachia kiasi flani hasa ukizingatia ulimwengu tunaoishi una changamoto nyingi sana na haziishi,sasa usipotoka na kukaa mbali na hayo maeneo,kwakweli unaweza kuona maisha yamesimama...
 
tuliondoka tanga usiku saa tisa mpaka saa kumi na mbili tukaanza kufika nungwi saa moja moja had saa mbili tukafika mkokoton halaf hatukufungiwa mashine jahazi lilikwenda na upepo lilifungwa tanga kama mashine ingefunga bas saa kumi na mbili tu tushatia nanga, speaking of experience yan nilipata si haba lakini huo usafiri unafaa wavuvi na wale walokwisha zoea kupiga makasia inatisha usijaribu labda ukaze roho

Mkuu hapo Nungwi ulipita na jahazi kweli una roho ngumu watu wanapita na meli tu hapatoshi bu the way hongera sana.......
 
Kusafiri ni advanture kwa kweli me napenda hasa kwa usafiri wa bus safari ninayoikumbuka ni ya kutoka Dar - são paulo, Brazil masaa 17 angani ilinikera kwa kuwa angani huoni kitu....another trip ni ndani ya Brazil kutoka mji wa São paulo kwenda Rio de janeiro niliipenda kwa kuwa nilisafiri kwa bus masaa 10
 
Mkuu hapo Nungwi ulipita na jahazi kweli una roho ngumu watu wanapita na meli tu hapatoshi bu the way hongera sana.......
haha ndio tulipita na jahazi ilikua ni kama nambeep Allah bahat siku zetu zilikua mbali tulifika salama
 
Back
Top Bottom