Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,321
- 18,574
Salaam wanabodi,
Awali nipongeze walipa kodi na waasisi wa wazo la ujenzi wa Sgr nchini. Japo ni mwanzo ila tuseme ukweli ili maboresho yafanyike. Natoa experience kwa reference ya kituo cha Dodoma nilipowahi kusafiri kuelekea Jijini Dsm.
Awali nipongeze walipa kodi na waasisi wa wazo la ujenzi wa Sgr nchini. Japo ni mwanzo ila tuseme ukweli ili maboresho yafanyike. Natoa experience kwa reference ya kituo cha Dodoma nilipowahi kusafiri kuelekea Jijini Dsm.
- Punguzeni matangazo ya kusifia Rais na Serikali kwa ujumla wake. Huu ni uchawa, huko wenzetu wanazo treni nyingi na nzuri lakini ukipanda huwezi kukuta haya mambo. After all Rais hajasimamia ujenzi kwa pesa yake kutoka mfukoni, bali kodi na mikopo itakayolipwa na watanzania. Msitumie usafiri wa umma kufanya kampeni za chama mjiheshimu.
- Madirisha ya wahudumu hayana watu pale ground floor, madirisha kibao mhudumu mmoja hii inapoteza muda.
- Fikirieni kuwa na kitu karibu na mji wa Serikali Mtumba au Ihumwa kwa treni ya express. Hizo ofisi zinatembelewa na wageni wengi sana sasa inaboa kidogo mtu anaenda Mji wa Serikali alafu anaenda kushuka mbele kisha arudi nyuma umbali wa zaidi ya kilomita 20.
- Angalieni namna ya watu kuruhusiwa kupanda na vyakula, kwenye ndege mtu anapanda mpaka na ndoo ya sato kutoka Mwanza ikiwa imefungwa vema, nyie kila kitu mnazuia. Angalieni namna ya kwenda nalo maisha lazima yawe simple. Wahudumu mlioajiri kuuza kahawa na bites wajinga wajinga pia, unampa mtu elfu tano anakwambia hana chenji na anaondoka na chai yake wala sio kutafuta chenji.
- Kukata tiketi mtandaoni unahitaji kupokea code kwenye namba yako ya simu, hii haina ulazima mbona mifumo mingi tu ya namna hii ipo na haihitaji namba ya simu? Imagine uko nje kidogo ya network ya Tanzania na unataka kumkatia mtu tiketi maana haiwezekani kwa sababu sms ya code haitakufikia. Jifunzeni kwenye usafiri wa anga hata mabasi. Vitu viwe simple.
- Kuuza vitu bei ghali kuliko uhalisia na bei ya soko. mfano korosho za 75g mnauza elfu 4. maana yake kilo moja mnauza elfu 53, kwamba zinatoka nje ya nchi au zinalimwa na Wamakonde wenzetu na isitoshe mnawalangua tu
