Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu umenena safi kabisa, tatizo ni kuwa baadhi ya mapungufu yamewekwa kutengeneza fursa kwa watu fulani ili watengeneze pesaSalaam wanabodi,
Awali nipongeze walipa kodi na waasisi wa wazo la ujenzi wa Sgr nchini. Japo ni mwanzo ila tuseme ukweli ili maboresho yafanyike. Natoa experience kwa reference ya kituo cha Dodoma nilipowahi kusafiri kuelekea Jijini Dsm.
- Punguzeni matangazo ya kusifia Rais na Serikali kwa ujumla wake. Huu ni uchawa, huko wenzetu wanazo treni nyingi na nzuri lakini ukipanda huwezi kukuta haya mambo. After all Rais hajasimamia ujenzi kwa pesa yake kutoka mfukoni, bali kodi na mikopo itakayolipwa na watanzania. Msitumie usafiri wa umma kufanya kampeni za chama mjiheshimu.
- Madirisha ya wahudumu hayana watu pale ground floor, madirisha kibao mhudumu mmoja hii inapoteza muda.
- Fikirieni kuwa na kitu karibu na mji wa Serikali Mtumba au Ihumwa kwa treni ya express. Hizo ofisi zinatembelewa na wageni wengi sana sasa inaboa kidogo mtu anaenda Mji wa Serikali alafu anaenda kushuka mbele kisha arudi nyuma umbali wa zaidi ya kilomita 20.
- Angalieni namna ya watu kuruhusiwa kupanda na vyakula, kwenye ndege mtu anapanda mpaka na ndoo ya sato kutoka Mwanza ikiwa imefungwa vema, nyie kila kitu mnazuia. Angalieni namna ya kwenda nalo maisha lazima yawe simple. Wahudumu mlioajiri kuuza kahawa na bites wajinga wajinga pia, unampa mtu elfu tano anakwambia hana chenji na anaondoka na chai yake wala sio kutafuta chenji.
- Kukata tiketi mtandaoni unahitaji kupokea code kwenye namba yako ya simu, hii haina ulazima mbona mifumo mingi tu ya namna hii ipo na haihitaji namba ya simu? Imagine uko nje kidogo ya network ya Tanzania na unataka kumkatia mtu tiketi maana haiwezekani kwa sababu sms ya code haitakufikia. Jifunzeni kwenye usafiri wa anga hata mabasi. Vitu viwe simple.
- Kuuza vitu bei ghali kuliko uhalisia na bei ya soko. mfano korosho za 75g mnauza elfu 4. maana yake kilo moja mnauza elfu 53, kwamba zinatoka nje ya nchi au zinalimwa na Wamakonde wenzetu na isitoshe mnawalangua tu
Kwenye ndege unaingia na ugali wako wa muhogo?Tunatofautiana kwenye matumizi ya chakula kulingana na afya ya mtu, wapo wasiotumia chumvi, mafuta, sukari, nyama na wanga kwa wingi.
Hayo ni maoni yako nayaheshimu Mkuu. ila kumbuka ukipanda na chakula sio lazima ule. unanunua zabibu za elfu 5 upelekee familia Dsm unaambiwa haziruhusiwi. Think againKupanda na vyakula ni BIG NO!
Msilete ushamba.
Na tukumbuke Express ni Express na siyo treni ya wafanyakazi wa serikali.
Unaweza kuniita mshamba kwa sababu hatufahamiani. Ila ujue tu madege nimepanda mpaka ya kutoka nje hili bara letu kwenda mabara mengine na nimejifunza mengi sana.Kwenye ndege sato wanakuwa eneo la mixogo sasa mshamba anataka single na sato na vyakula eneo la abiria hiyo kiboko
Katika fikira zako chakula ni ugali tu?Kwenye ndege unaingia na ugali wako wa muhogo?
Zikiwekwa standards of service, tusipende kuzi cheapen kwa sabababu zisizo na msingi.Katika fikira zako chakula ni ugali tu?
ukinunua zabibu zikafungwa vizuri kwenye kiboksi unatoka Dodoma unaenda Dsm ukazibeba kuna ubaya gani? na isitoshe zinauzwa pale pale stesheni.
Pointi ya msingi ni ku-regulate vyakula gani vipande kama mzigo tu wanaweza tenga sehemu maalumu.
Ndugu yangu unaweza kupanda Ethiopia Airline na ndoo ya samaki frozen, kwanini usipande na ndoo ya samaki frozen kwenye sgr? ni utaratibu tu.
Hata wewe unayepinga hapa siku Sgr wakiboresha hili utakuwa wa kwanza kubeba parcels kupelekea familia yako zawadi, Watanzania ndivyo tulivyo
Haukatazwi, mbona watu wanasafiri na vyakula kwenye ATC toka mikoani.Kwenye ndege unaingia na ugali wako wa muhogo?
Unaboa! Huu ni ukauzu tuSalaam wanabodi,
Awali nipongeze walipa kodi na waasisi wa wazo la ujenzi wa Sgr nchini. Japo ni mwanzo ila tuseme ukweli ili maboresho yafanyike. Natoa experience kwa reference ya kituo cha Dodoma nilipowahi kusafiri kuelekea Jijini Dsm.
- Punguzeni matangazo ya kusifia Rais na Serikali kwa ujumla wake. Huu ni uchawa, huko wenzetu wanazo treni nyingi na nzuri lakini ukipanda huwezi kukuta haya mambo. After all Rais hajasimamia ujenzi kwa pesa yake kutoka mfukoni, bali kodi na mikopo itakayolipwa na watanzania. Msitumie usafiri wa umma kufanya kampeni za chama mjiheshimu.
- Madirisha ya wahudumu hayana watu pale ground floor, madirisha kibao mhudumu mmoja hii inapoteza muda.
- Fikirieni kuwa na kitu karibu na mji wa Serikali Mtumba au Ihumwa kwa treni ya express. Hizo ofisi zinatembelewa na wageni wengi sana sasa inaboa kidogo mtu anaenda Mji wa Serikali alafu anaenda kushuka mbele kisha arudi nyuma umbali wa zaidi ya kilomita 20.
- Angalieni namna ya watu kuruhusiwa kupanda na vyakula, kwenye ndege mtu anapanda mpaka na ndoo ya sato kutoka Mwanza ikiwa imefungwa vema, nyie kila kitu mnazuia. Angalieni namna ya kwenda nalo maisha lazima yawe simple. Wahudumu mlioajiri kuuza kahawa na bites wajinga wajinga pia, unampa mtu elfu tano anakwambia hana chenji na anaondoka na chai yake wala sio kutafuta chenji.
- Kukata tiketi mtandaoni unahitaji kupokea code kwenye namba yako ya simu, hii haina ulazima mbona mifumo mingi tu ya namna hii ipo na haihitaji namba ya simu? Imagine uko nje kidogo ya network ya Tanzania na unataka kumkatia mtu tiketi maana haiwezekani kwa sababu sms ya code haitakufikia. Jifunzeni kwenye usafiri wa anga hata mabasi. Vitu viwe simple.
- Kuuza vitu bei ghali kuliko uhalisia na bei ya soko. mfano korosho za 75g mnauza elfu 4. maana yake kilo moja mnauza elfu 53, kwamba zinatoka nje ya nchi au zinalimwa na Wamakonde wenzetu na isitoshe mnawalangua tu
Huu ugonjwa alituachia Mzee babaHapo namba 01 umenikosha kiongozi..Yaani UCHAWA umekuwa tatizo kubwa kwa sasa..sijui ipo kwenye Job description ya kila Taasisi na wateule wote??..yaani kama miKASUKU..ujinga
Kumbe ile chai ya wizi ni kote hahaha nilijua ni mimi tu nimepigwa!!Uko sahihi, upumbavu wa kuwekeana royal tour mwanzo mpaka mwisho wa safari unakera sana.
Alafu ile chai yao ni wizi, kikopo kidogo na bado wanakupa nusu! Unabaki unajiuliza hivi kuibia watu ni sifa?
Nchi ya hovyo sana hii mkuuHii tabia ya matangazo ya kumsifu rais inakera sana.kiufupi hii sifia sifia ya rais inatufedhehesha sana watanzania tunaojitambua
Safi sana, hii ndio maana ya think tank.Kuwa na kitu karibu na mji wa Serikali Mtumba au Ihumwa kwa kuwa na train ya expres, huo ni mpango maalumu ambao unahitaji fedha baada ya mradi mzima kukamilika na ni mpango maalumu unaojitegemea (Ni project), lakini siyo kwa sababu ya watu watokao Dar es salaam kuja kituoni, kwa maana ya "Kushukia mbele halafu wanarudi nyuma" hiyo haitakuwa sababu ya msingi ya kuwa na train ya express, kwa kuwa hakuna "Mbele ya kituo au nyuma ya kituo" ukiwa jijini Dodoma.
Kwa kuwa baada ya mradi kukamilika kuna wasafiri ambao watakuwa wanatoka Mwanza, Kigoma na Tabora kuja Dodoma na hatimae wanatakiwa kwenda mji wa Serikali watakuwa wameshukia "Mbele ya kituo au nyuma ya kituo?"
Kumbuka kile kituo hakina mbele wala nyuma ya mahali unakoenda ile ni Destnation, baada ya kufika kituoni haijalishi unaenda wapi unalazimika kukodi usafiri, kupanda usafiri wa pamoja au utembee kwa mguu ili ufike uendako.
Wewe umeangalia upande mmoja tu kwa maana ya taasisi hiyo ya mji wa Serikali, hujaangalia taasisi zingine kama Benjamini Mkapa hosptal, uwanja wa ndege mpya unaojengwa Dodoma na taasisi zingine, na wasafiri watakaoshukia kituoni hapo ambao hawaendi kwenye taasisi hiyo ya mji wa Serikali, watakuwa wanaenda mbele au wanarudi nyuma!
Kula nyumbani kwako kabisa kabla ya safari au nunuwa snacks na maji hakuna atakayekuzia.Tunatofautiana kwenye matumizi ya chakula kulingana na afya ya mtu, wapo wasiotumia chumvi, mafuta, sukari, nyama na wanga kwa wingi.