TRC boresheni haya, nimepanda treni yenu ni nzuri ila tunahitaji maboresho zaidi

TRC boresheni haya, nimepanda treni yenu ni nzuri ila tunahitaji maboresho zaidi

kwente ticket trc watumie mfumo wa mabasi uko efficient sana
 
Salaam wanabodi,
Awali nipongeze walipa kodi na waasisi wa wazo la ujenzi wa Sgr nchini. Japo ni mwanzo ila tuseme ukweli ili maboresho yafanyike. Natoa experience kwa reference ya kituo cha Dodoma nilipowahi kusafiri kuelekea Jijini Dsm.
  1. Punguzeni matangazo ya kusifia Rais na Serikali kwa ujumla wake. Huu ni uchawa, huko wenzetu wanazo treni nyingi na nzuri lakini ukipanda huwezi kukuta haya mambo. After all Rais hajasimamia ujenzi kwa pesa yake kutoka mfukoni, bali kodi na mikopo itakayolipwa na watanzania. Msitumie usafiri wa umma kufanya kampeni za chama mjiheshimu.
  2. Madirisha ya wahudumu hayana watu pale ground floor, madirisha kibao mhudumu mmoja hii inapoteza muda.

  3. Fikirieni kuwa na kitu karibu na mji wa Serikali Mtumba au Ihumwa kwa treni ya express. Hizo ofisi zinatembelewa na wageni wengi sana sasa inaboa kidogo mtu anaenda Mji wa Serikali alafu anaenda kushuka mbele kisha arudi nyuma umbali wa zaidi ya kilomita 20.
  4. Angalieni namna ya watu kuruhusiwa kupanda na vyakula, kwenye ndege mtu anapanda mpaka na ndoo ya sato kutoka Mwanza ikiwa imefungwa vema, nyie kila kitu mnazuia. Angalieni namna ya kwenda nalo maisha lazima yawe simple. Wahudumu mlioajiri kuuza kahawa na bites wajinga wajinga pia, unampa mtu elfu tano anakwambia hana chenji na anaondoka na chai yake wala sio kutafuta chenji.
  5. Kukata tiketi mtandaoni unahitaji kupokea code kwenye namba yako ya simu, hii haina ulazima mbona mifumo mingi tu ya namna hii ipo na haihitaji namba ya simu? Imagine uko nje kidogo ya network ya Tanzania na unataka kumkatia mtu tiketi maana haiwezekani kwa sababu sms ya code haitakufikia. Jifunzeni kwenye usafiri wa anga hata mabasi. Vitu viwe simple.
  6. Kuuza vitu bei ghali kuliko uhalisia na bei ya soko. mfano korosho za 75g mnauza elfu 4. maana yake kilo moja mnauza elfu 53, kwamba zinatoka nje ya nchi au zinalimwa na Wamakonde wenzetu na isitoshe mnawalangua tu
Ndugu umenena safi kabisa, tatizo ni kuwa baadhi ya mapungufu yamewekwa kutengeneza fursa kwa watu fulani ili watengeneze pesa
 
Kupanda na vyakula ni BIG NO!
Msilete ushamba.
Na tukumbuke Express ni Express na siyo treni ya wafanyakazi wa serikali.
Hayo ni maoni yako nayaheshimu Mkuu. ila kumbuka ukipanda na chakula sio lazima ule. unanunua zabibu za elfu 5 upelekee familia Dsm unaambiwa haziruhusiwi. Think again
 
Kwenye ndege sato wanakuwa eneo la mixogo sasa mshamba anataka single na sato na vyakula eneo la abiria hiyo kiboko
Unaweza kuniita mshamba kwa sababu hatufahamiani. Ila ujue tu madege nimepanda mpaka ya kutoka nje hili bara letu kwenda mabara mengine na nimejifunza mengi sana.

Waweke sehemu ya parcels, treni ni yetu waboreshe. Huko kwa wenzetu imewezekanaje? Think on it
 
Nimeangalia wingi watanzania wanaosafiri kwenda kwenye mji wa serikali kutafuta huduma.
Tukiongeza consideration ya Hospital ya Benjamini mkapa bado ilipo stesheni ni mbali sana.
Badala ya kupinga pinga kila kitu, TRC watafanya analysis wenyewe. Ninachoamini inawezekana kuweka kituo eneo ambalo sio mbali na mji wa Serikali ili kurahisisha huduma kwa watanzania na wageni wote wanaosafiri kwenda kwenye hizo Wizara kupata huduma.
 
Kwenye ndege unaingia na ugali wako wa muhogo?
Katika fikira zako chakula ni ugali tu?
ukinunua zabibu zikafungwa vizuri kwenye kiboksi unatoka Dodoma unaenda Dsm ukazibeba kuna ubaya gani? na isitoshe zinauzwa pale pale stesheni.

Pointi ya msingi ni ku-regulate vyakula gani vipande kama mzigo tu wanaweza tenga sehemu maalumu.

Ndugu yangu unaweza kupanda Ethiopia Airline na ndoo ya samaki frozen, kwanini usipande na ndoo ya samaki frozen kwenye sgr? ni utaratibu tu.

Hata wewe unayepinga hapa siku Sgr wakiboresha hili utakuwa wa kwanza kubeba parcels kupelekea familia yako zawadi, Watanzania ndivyo tulivyo
 
Zikiwekwa standards of service, tusipende kuzi cheapen kwa sabababu zisizo na msingi.
Otherwise mabasi bado yapo, kapande kule.
 
Hivi ni sahihi kusema Treni yenu au Treni yetu? Ukizingatia kodi yetu ..
 
Umetoa mapendekezo mazuri sana na ya muhimu pia. Hilo pendekezo namba 1 kwa kweli lina chefua sana
 
Uko sahihi, upumbavu wa kuwekeana royal tour mwanzo mpaka mwisho wa safari unakera sana.
Alafu ile chai yao ni wizi, kikopo kidogo na bado wanakupa nusu! Unabaki unajiuliza hivi kuibia watu ni sifa?
 
Salaam wanabodi,
Awali nipongeze walipa kodi na waasisi wa wazo la ujenzi wa Sgr nchini. Japo ni mwanzo ila tuseme ukweli ili maboresho yafanyike. Natoa experience kwa reference ya kituo cha Dodoma nilipowahi kusafiri kuelekea Jijini Dsm.
  1. Punguzeni matangazo ya kusifia Rais na Serikali kwa ujumla wake. Huu ni uchawa, huko wenzetu wanazo treni nyingi na nzuri lakini ukipanda huwezi kukuta haya mambo. After all Rais hajasimamia ujenzi kwa pesa yake kutoka mfukoni, bali kodi na mikopo itakayolipwa na watanzania. Msitumie usafiri wa umma kufanya kampeni za chama mjiheshimu.
  2. Madirisha ya wahudumu hayana watu pale ground floor, madirisha kibao mhudumu mmoja hii inapoteza muda.

  3. Fikirieni kuwa na kitu karibu na mji wa Serikali Mtumba au Ihumwa kwa treni ya express. Hizo ofisi zinatembelewa na wageni wengi sana sasa inaboa kidogo mtu anaenda Mji wa Serikali alafu anaenda kushuka mbele kisha arudi nyuma umbali wa zaidi ya kilomita 20.
  4. Angalieni namna ya watu kuruhusiwa kupanda na vyakula, kwenye ndege mtu anapanda mpaka na ndoo ya sato kutoka Mwanza ikiwa imefungwa vema, nyie kila kitu mnazuia. Angalieni namna ya kwenda nalo maisha lazima yawe simple. Wahudumu mlioajiri kuuza kahawa na bites wajinga wajinga pia, unampa mtu elfu tano anakwambia hana chenji na anaondoka na chai yake wala sio kutafuta chenji.
  5. Kukata tiketi mtandaoni unahitaji kupokea code kwenye namba yako ya simu, hii haina ulazima mbona mifumo mingi tu ya namna hii ipo na haihitaji namba ya simu? Imagine uko nje kidogo ya network ya Tanzania na unataka kumkatia mtu tiketi maana haiwezekani kwa sababu sms ya code haitakufikia. Jifunzeni kwenye usafiri wa anga hata mabasi. Vitu viwe simple.
  6. Kuuza vitu bei ghali kuliko uhalisia na bei ya soko. mfano korosho za 75g mnauza elfu 4. maana yake kilo moja mnauza elfu 53, kwamba zinatoka nje ya nchi au zinalimwa na Wamakonde wenzetu na isitoshe mnawalangua tu
Unaboa! Huu ni ukauzu tu
 
Hapo namba 01 umenikosha kiongozi..Yaani UCHAWA umekuwa tatizo kubwa kwa sasa..sijui ipo kwenye Job description ya kila Taasisi na wateule wote??..yaani kama miKASUKU..ujinga
Huu ugonjwa alituachia Mzee baba
 
Uko sahihi, upumbavu wa kuwekeana royal tour mwanzo mpaka mwisho wa safari unakera sana.
Alafu ile chai yao ni wizi, kikopo kidogo na bado wanakupa nusu! Unabaki unajiuliza hivi kuibia watu ni sifa?
Kumbe ile chai ya wizi ni kote hahaha nilijua ni mimi tu nimepigwa!!
Yani chai ya rangi ya buku kikopo kidogo na bado wakaweka nusu?? Nilishangaa sana

Sent from my SM-A325N using JamiiForums mobile app
 
Kuwa na kitu karibu na mji wa Serikali Mtumba au Ihumwa kwa kuwa na train ya expres, huo ni mpango maalumu ambao unahitaji fedha baada ya mradi mzima kukamilika na ni mpango maalumu unaojitegemea (Ni project), lakini siyo kwa sababu ya watu watokao Dar es salaam kuja kituoni, kwa maana ya "Kushukia mbele halafu wanarudi nyuma" hiyo haitakuwa sababu ya msingi ya kuwa na train ya express, kwa kuwa hakuna "Mbele ya kituo au nyuma ya kituo" ukiwa jijini Dodoma.

Kwa kuwa baada ya mradi kukamilika kuna wasafiri ambao watakuwa wanatoka Mwanza, Kigoma na Tabora kuja Dodoma na hatimae wanatakiwa kwenda mji wa Serikali watakuwa wameshukia "Mbele ya kituo au nyuma ya kituo?"

Kumbuka kile kituo hakina mbele wala nyuma ya mahali unakoenda ile ni Destnation, baada ya kufika kituoni haijalishi unaenda wapi unalazimika kukodi usafiri, kupanda usafiri wa pamoja au utembee kwa mguu ili ufike uendako.

Wewe umeangalia upande mmoja tu kwa maana ya taasisi hiyo ya mji wa Serikali, hujaangalia taasisi zingine kama Benjamini Mkapa hosptal, uwanja wa ndege mpya unaojengwa Dodoma na taasisi zingine, na wasafiri watakaoshukia kituoni hapo ambao hawaendi kwenye taasisi hiyo ya mji wa Serikali, watakuwa wanaenda mbele au wanarudi nyuma!
Safi sana, hii ndio maana ya think tank.
 
Tunatofautiana kwenye matumizi ya chakula kulingana na afya ya mtu, wapo wasiotumia chumvi, mafuta, sukari, nyama na wanga kwa wingi.
Kula nyumbani kwako kabisa kabla ya safari au nunuwa snacks na maji hakuna atakayekuzia.

Safari ya masaa machache unataka kula nini? Si utakula unachotaka ukifika?

Mimi hata safari ya masaa 12 bus likisimama sehemu ya chakula huwa nanunuwa clips na maji na juice tuz sili chakula njiani.
 
Mimi namba 1, hivi Watanzania tuna nini? Yaani kuanzia viongozi lazima wasifie Raisi, sasa kwenye usafiri wa umma mnaleta hayo. Niyeye katoa hela yake kutujengea hiyo SGR?
Mkitaka kusifia, tajeni kila jina la mlipa kodi katika hii nchi. Huyo mnayemsifia visivyosifika hauziki, msituchoshe.
 
Back
Top Bottom