KERO TRC boresheni miundombinu katika Vyoo vya Kituo cha SGR - Dar

KERO TRC boresheni miundombinu katika Vyoo vya Kituo cha SGR - Dar

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Moja kati ya vitu ambavyo nilikuwa najiuliza ni kama Watanzania tunaweza kutunza Miundombinu yetu ya Reli ya SGR, bila unafiki ukiitazama imekaa poa kwa asilimia kubwa.

WhatsApp Image 2024-10-18 at 17.45.44_66205655.jpg

Lakini jioni ya leo Oktoba 18, 2024 wakati najiandaa kusafiri na usafiri huo nilipoingia kwenye Choo cha Kituo cha SGR Dar ambayo nasikia inaitwa John P Magufuli Station, nimekutana na hali ambayo inaonesha sio mwanzo mzuri.

Nimepiga picha hii inaoonesha tayari kumeanza kuchangamka, kama inavyoonekana hapo sinki mojawapo limefungwa halitakiwi kutumika.

Soma Pia: Miundombinu ya mabomba kwenye Vyoo vya 'Magufuli Bus Terminal' imeharibika, maji yanatoka ovyo na hakuna anayejali

Kingine kinachokera, yaani chooni hakuna papers za kujifuta ukimaliza kunawa, unaondoka na maji yako kama ilivyo vyoo vya Uswahilini.

====== =====

MAJINA YA VITUO VYA SGR TANZANIA
👉Dar Es salaam - John P Magufuli Station
👉Morogoro - Jakaya Kikwete Station
👉Dodoma - Samia Suluhu Station
👉Tabora - Ally Hassan Mwinyi Station
👉Shinyanga - Abeid Aman Karume Station
👉Mwanza - Julius Kambarage Nyerere Station
👉Kigoma - Benjamin Mkapa Station
 
Baadhi ya watanzania wana tabia za ajabu sana. Wana matumizi mabaya sana ya vyoo hasa hivi vya umma.
 
Inatakiwa TRC wakamate na wapige faini abilia wanaoharibu miundo halafu wawatangaze kwenye tv na mitandao ya kijamii kwani kule mwendokasi na airport wanawezaje
 
Hata wakiweka tissue mswahili anaondoka nayo yote
Hapo una bahati hata hiyo sink bado ipo
Ni laana ya wengi kutokuwa na malezi mazuri
Ila na serkali ni wajibu wao kuwa na watu 24/7 wakisafisha na kuhakikisha vyoo visafi vina maji kila wakati
Mbona Airport wanajitahidi au kwa sababu wanaona watatangazwa kwenye mitandao na foreigners?
 
Moja kati ya vitu ambavyo nilikuwa najiuliza ni kama Watanzania tunaweza kutunza Miundombinu yetu ya Reli ya SGR, bila unafiki ukiitazama imekaa poa kwa asilimia kubwa.

Lakini jioni ya leo Oktoba 18, 2024 wakati najiandaa kusafiri na usafiri huo nilipoingia kwenye Choo cha Kituo cha SGR Dar ambayo nasikia inaitwa John P Magufuli Station, nimekutana na hali ambayo inaonesha sio mwanzo mzuri.

Nimepiga picha hii inaoonesha tayari kumeanza kuchangamka, kama inavyoonekana hapo sinki mojawapo limefungwa halitakiwi kutumika.

Soma Pia: Miundombinu ya mabomba kwenye Vyoo vya 'Magufuli Bus Terminal' imeharibika, maji yanatoka ovyo na hakuna anayejali

Kingine kinachokera, yaani chooni hakuna papers za kujifuta ukimaliza kunawa, unaondoka na maji yako kama ilivyo vyoo vya Uswahilini.

====== =====

MAJINA YA VITUO VYA SGR TANZANIA
👉Dar Es salaam - John P Magufuli Station
👉Morogoro - Jakaya Kikwete Station
👉Dodoma - Samia Suluhu Station
👉Tabora - Ally Hassan Mwinyi Station
👉Shinyanga - Abeid Aman Karume Station
👉Mwanza - Julius Kambarage Nyerere Station
👉Kigoma - Benjamin Mkapa Station
Mara hii!
 
Vyooni Kuna mashine za kukaushia Mikono tissue ya nin?
Kwahiyo kama choo kimepata hitilafu kiachwe kitumike
 
Ni aibu hata kwa kadogosa kuzungumzia mambo ya choo

Ova
 
Ukute Kuna mtu wa Dini Fulani, aliingia na jiwe, alipomaliza kulitumia ktk haja akalirusha humo hivyo choo kuziba!!
 
Ndio maana hata ukienda hotel za kitalii na mwanaume wa kibongo mnapandishiwa bei na wanawawekea camera za siri chooni

wabongo hovyo
Au kaburu alivyofanya kutenga sehemu ya za waafrika na sehemu za wazungu ambazo weusi ni marufuku. Ila hao TRC ni kama CCM tu. Unapåojenga vyoo vya umma ni lazima ujue jamii itakayotumia ikoje na ujiandae.
 
Management na utunzaji wabongo ni sifuri kabisa.
 
Hapo sheria kali haswa zitungwe kwa hao wapumbavu waharibifu, jitu makusudi linang'oa koki, linajisaidia haja kubwa pembeni, mengine yamejazana mitaani huku yanajisaidia hovyo mijini na kutupa taka kwenye mitaro
Hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom