TRC: Huduma ya Treni ya Arusha - Dar imerejea, ilisimama kutokana na sehemu ya njia ya reli kujaa maji

TRC: Huduma ya Treni ya Arusha - Dar imerejea, ilisimama kutokana na sehemu ya njia ya reli kujaa maji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk amezungumzia taarifa kuwa Treni inayofanya safari zake Dar es Salaam – Arusha ‘imekufa’ na haitaendelea kuwepo kama ilivyokuwa ikidaiwa na baadhi ya Wadau.

Anafafanua kilichotokea hadi huduma hiyo kusimama, anasema:

"Huduma za Treni hiyo hazijazimama moja kwa moja kama inavyoelezwa, kuna sehemu korofi ambayo kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha hapo kati eneo hilo lilikuwa linajaa maji kiasi cha kufunika reli, kwa hali hiyo huwezi kupitisha treni.

"Tukaamua kuisubirisha kwanza, tukiona njia sio salama kwa abiria huwa tunadiriki hata kurudisha nauli lakini lakini sio kuhatarisha maisha ya Watu.

"Kuhusu tiketi kutopatikana kwenye mfumo wa ukataji tiketi wakati huo, kunapokuwa na changamoto kama hiyo ya usafiri kukosekana huwezi kuendelea kuweka ratiba iwe vilevile kwenye mtandao."

Pia soma ~ Treni ya Dar-Tanga-Arusha imekwama, wanaohusika watoe mwongozo wa nini kinaendelea
 
Back
Top Bottom