Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Itakumbukwa mnamo Desemba 24, 2024, TRC ilitoa taarifa ya kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam na kupokelewa kwa mabehewa ya mizigo 264 yaliyotengenezwa China kwa ajili ya reli ya kisasa (SGR).
Katika taarifa iliyotolewa hivi karibuni na TRC, ilieleza kwamba zoezi la majaribio ambalo lilitakiwa kuanza kufanyika kabla operesheni rasmi za kusafirisha miziko limekamilika vyema kama ilivyotakiwa.
Kufuatia kukamilika kwa zoezi hilo Ofisa uhusiano wa Shirika la Reli (TRC), Fred Mwanjala, leo Machi 26, 2025 akizungumza na chanzo cha taarifa hii, amesema kwamba mnamo Mwezi June operesheni za kusafirisha mizigo kwenda Dodoma itaanza rasmi.
TRC ilieleza kwamba katika mabehewa hayo, 200 yameundwa kwa ajili ya kubeba makontena, huku 64 yakibeba mizigo isiyofungwa (shehena kichele).