TRC mnazidi kufeli kila uchwao.

Kuna ubaya gani kuwa na BACK UP? tena TRC walifanya kosa kutoleta hizo diesel engine kwa ajili ya backup. Muhimu ni speed, hata hizo za diesel zikija speed itakuwa ile ile waliyodesign. Huwezi kufananisha na zile treni za kigoma. Imesemwa hapo za diesel zitatumika iwapo kuna tatizo la umeme shida iko wapi? Mlitaka iwapo umeme ukikatika watu walale njiani mpate thread jf na kwenye mitandao mingine?
 
CCM Hoyeee
 
Mama alidandia ishu hazikua zake. Ajabu ni pale anapo ng'ang'ania Ili atupeleke chaka
 
Huyu Masanja ni tapeli si alituaeleza kuwa hizo treni zina power bank ya kuitunza umeme ata ukikatika umeme wa Tanesco linaendelea na safari!🤣🤣🤣🤣
 
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema kwa kipindi cha muda mfupi mpaka kufikia July 28, 2024.Treni hiyo ya kisasa ilikuwa imekwisha safirisha abiria wapatao 28,600 na kukusanya kiasi cha fedha za Kitanzania Shilingi Milioni 744 toka kuanza kwa safari hizo.

Hata hivyo baadhi ya Wachumi wameonyesha wasiwasi juu ya hitilafu ya umeme iliyojitokeza wakati wa safari ya majaribio iliyopelekea Treni kusimama kwa muda wa masaa mawili na baadae Shirika la Reli Tanzania wakatoa ripoti ya awali kuwa hitilafu hiyo ilisababishwa na Ngendere na Ndege aina ya Bundi.

Suala ambalo Dkt Ntui Ponsian Mhadhiri kutoka katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza, amesema Shirika la Reli la Tanzania linapaswa kujiepusha na utoaji wa kauli kama hizo kwakuwa kauli hizo zinaweza kupelekea wateja na wananchi kupoteza imani na huduma zinazotolewa na shirika hilo.
 
Takataka kabisa hili shirika
Once a failure , always a failure
 
JK alisema wakati wa utawala wake SGR ilikuwa ijengwe ya treni za Diesel ⛽ ila Magufuli alipoingia ndiyo akasema atajenga SGR ya umeme.
Connect the dots;wamiliki wa sheli,malori na mabasi ni akaina nani!!!
 
Rais Samia amewatoa wasiwasi wa kukosa abiria wawekezaji waliowekeza katika sekta binafsi upande wa usafirishaji kwa njia ya Mabasi kwa kutoa ruhusa kwa wawekezaji hao kutafuta namna ya kuingia ubia na shirika la Reli Tanzania kutengeneza mfumo utakaowawezesha abiria kusafiri kwa kutumia tiketi moja kuunganisha safari katika Mabasi yanayokwenda katika mikoa mingine.
 

Hapa sasa ndio watu wataelewa. tuliambiwa sasa kukatika umeme ni historia. Bwawa la mwalimu Nyerere.. kiko wapi? Hawa ni kikundi cha wezi wezi wezi tu.
 
Mtanzania hodari kwa kuiba tu
Na kutengeneza figisufigisu tu zaidi ya hapo hakuna kitu

Ova
 
Kwa ujinga huu diesel haiwezi kukosa? huko tusifike,wahakikishe Kwa namna yoyote umeme uwepo tu wa kutosha.magu alisema tumechelewa mno wahuni mmeona fursa hapo?
 
Kwa ujinga huu diesel haiwezi kukosa? huko tusifike,wahakikishe Kwa namna yoyote umeme uwepo tu wa kutosha.magu alisema tumechelewa mno wahuni mmeona fursa hapo?
Umeme wa kutosha upo. Unafikiri umeme unakatika kwa sababu hautoshi? Inawezekana hujui kuwa umeme kukatika sio lazima kuwe na upungufu.
 

We jamaa ni mnafiki sana. Angalia hii comment yako ya February wakati Kadogosa anazungumzia ujio wa vichwa vya dizeli. Angalia na hii ya leo.. full unafki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…