Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanzisha mpango wa kununua injini za dizeli ili kuhakikisha huduma ya usafiri wa reli ya kisasa (SGR) bila kikwazo endapo umeme utakatika.
View attachment 3175720
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, amethibitisha hilo na kuelezea kuwa tayari kampuni moja imebainishwa kuzalisha injini hizo.
View attachment 3175721
Huduma ya reli kutoka Dar hadi Morogoro imekuwa ikikumbwa na changamoto ya umeme mara kadhaa na kusababisha abiria kukwama safarini kabla ya kufika wanakokwenda.
-------------------------------------------
Taarifa hii inakuwa mwiba mkali sana kwa machawa na wale wazee wa mapambio. Mkipewa mawazo na watu sio kila wakati mnatakiwa kuwaona ni wapinzani. Sanja boy umefeli sana wewe pamoja na timu yako.
View attachment 3175722
Mlipoambiwa kuwa mnakwend kufanya project ambayo baadaye mtarudi kule kule, mliwaona wakosoaji ni chadema. Mlisema na kuwaaminisha watanzania kuwa umeme ni wa uhakika na treni hazitopata tatizo la kukatika.
Enewei nyie ndo wateulewa Rais! Wote tuseme kwa sauti moja kuwa MAMA ANAUPIGA MWINGI! Tusubirie machapisho na hongera nyingi kwa TRC