Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 221
- 542
Sitaki kusema natabiri ila napenda kuwatadharisha shirika la reli wawe makini na SGR, hayo makosa madogo madogo ya hii train kusimama simama bila kuelewa sababu za msingi, mara wakati mwingine utasikia umeme umekatika, kuweni makini ipo siku hii train itakataa kusimama, sijui kitakachotokea hapo lakini tunaomba tusisikie kuwa kazi ya Mungu haina makosa.
Train imenunuliwa kwa pesa za watanzania, hatujui kama tumepigwa au hatujapigwa ila tumewakabidhi nyinyi TRC muhisimamie ilete matokeo tunayotarajia na ituletee heshima katika nyanja ya usafirishaji barani Afrika. Tumeanza kuona tukimwagiwa sifa na nchi za jirani kuwa tumepiga hatua, wanasema Tanzania sasa ni nchi ya kupigiwa mfano ila hichi kinachoendelea hapa kila siku train kuzimazima na kusimamasimama ni aibu.
Tunaanza kuaibishana sasa, mwisho wa siku maintenance itatushinda kama ilivotokea kwa mabasi ya mwendo kasi. Mabasi yananunuliwa kibao unayakuta yard mengine yamelala eti kisa bolt moja hakuna na anayetakiwa kusaini amesafiri mwezi mzima.
Mama Samia tunaomba utoe tamko lako la kiuongozi kwa watu wa TANESCO NA TRC, wasilete utani na SGR hii ni investment yetu kubwa na tunatakata ufanisi siyo blabla na excuse za kila siku.