Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 450
- 3,368
Behewa namba 14 kwenye treni ya Mwendokasi halina hewa.
Kwa mujibu wa mhudumu, tangu asubuhi, leo Oktoba 3, 2025 behewa hili limepata hitilafu na halijatengenezwa hadi sasa na hawajui litatengenezwa lini.
Hii imeleta adha kubwa kwa wasafiri wanaotumia jioni hii maana behewa limejaa, hakuna taa, hakuna AC, hakuna hewa. Watu wameomba kushuka maana wana suffocate lakini mlango umefungwa bila kusikilizwa na treni ipo njiani kuelekea Dar es Salaam.
Bahati mbaya wapo hadi wajawazito na watoto wadogo ambao changamoto hii inawaathiri sana.
Soma Pia: SGR yaanza kupoteza Ustaarabu, inaruhusu watu kulewa ndani ya treni na kusababisha kero kwa wengine
TRC, huu ni uzembe. Mtaua watu, huwezi kubeba watu kwenye behewa lenye giza, ambalo pia halina hewa. Wakipata madhara mtasema nini?
Mbaya zaidi hamjatoa hata taarifa kwa wasafiri, hata radhi hamuombi, ni hadi watu wapige kelele ndipo mnaanza kuja na sababu zenu zisizo eleweka.
Kwa tunaojiweza kiuchumi tumeamua bora tubaki Dodoma kuliko kukubali kufia njiani, bora kufanya utaratibu mwingine wa safari. Nawahurumia sana walioendelea na safari hii.
Naripoti kutoka milima ya Omatako, Namibia.
Mrejesho: Behewa namba 14 la SGR lilikokuwa bovu limetengenezwa, mambo yamenyooka