Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Siku moja baada ya taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro kutoa ripoti inayoonyesha kuwepo kwa abiria wenye lengo la kuhujumu Shirika Hilo hatimaye Leo Shirika la Reli (TRC) Limekiri kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu kwa baadhi ya abiria wa Treni ya umeme (SGR) kwa kukata tiketi za kushuka njiani na baadae kupitiliza vituo wanavyopaswa kushuka ikiwa ni nje ya thamani ya fedha zao.
Akizingumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa TRC Jamila Mbarouk amesema Walipata taarifa kutoka kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuwa kuna abiria wanafanya udanganyifu huo hivyo TRC imechukua hatua kadhaa ikiwemo kuimarisha ukaguzi wa tiketi.
"Eneo utakalopandia treni utascan tiketi yako,ndani ya treni pia wakaguzi wanafanya ukaguzi wa tiketi pia wakati wa kushuka unatakiwa kuscani ili kubaini kama kuna udanganyifu wowote, kama itakuwa kuna abiria kafanya udanganyifu basi alarm zitapiga kelele hivyo walinzi watakuja kuangalia kuna shida gani".
Ameongeza kuwa Abiria hususani wanaopanda katikati ya safari kuanzia stesheni ya ruvu na ngelengele ndio wengi wanafanya udanganyifu huo ambapo TRC kwa kushirikiana na vyombo vya usalama tayari wamewakamata baadhi ya abiria hao na kuwafikisha Mahakani,Pia katika sakata hilo TRC imewakamata watu kadhaa waliokuwa wanakata tiketi nyingi kwa wakati mmoja na kwenda kufanya udanganyifu.
Aidha ameongeza Kuwa tayari baaadhi ya abiria wanaofanya udanganyifu huo wameshatiwa mbaroni na wengine kufikishwa mahakamani huku wengine wakipiga faini ya kulipa mara mbili zaidi ya nauli waliopaswa kulipa
"tunafanya haya yote kuhakikisha mali ya umma wa Watanzania haipotei hivi hivi kwani ni wajibu wetu wote kulitunza Shirika kwa kulipa nauli stahiki" amesema
Pia soma DOKEZO - Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu
Jamila ameongeza kuwa Kwasasa ili kupanda treni ya SGR ni lazima uwe na kitambulisho chochote kinachoonesha sura ya muhusika na jina lake kamili ambalo pia litafanana na lile ambalo limeandikwa kwenye tiketi yake ili kudhibiti udanganyifu kwani pia kulibainika kuwepo kwa watu ambao walikuwa wakinunua tiketi nyingi ambazo hawakujulikana wanakozipeleka ambao nao tayari wametiwa nguvuni.
Aidha amewataka abiria kuwa waadilifu kwa kulinda mali ya umma na kuhakikisha kila mtu anakuwa mlinzi wa mwenzake kwa kuwafichua wanaohujumu na kusisitiza kuwa kwa yoyote atakayebainika kuhujumu shiriaka atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Source: HABARI 101 TZ Blog