TRC: Tumewakamata Watu kadhaa waliokuwa wanafanya ulanguzi wa tiketi za SGR na kufanya udanganyifu

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Siku moja baada ya taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro kutoa ripoti inayoonyesha kuwepo kwa abiria wenye lengo la kuhujumu Shirika Hilo hatimaye Leo Shirika la Reli (TRC) Limekiri kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu kwa baadhi ya abiria wa Treni ya umeme (SGR) kwa kukata tiketi za kushuka njiani na baadae kupitiliza vituo wanavyopaswa kushuka ikiwa ni nje ya thamani ya fedha zao.

Akizingumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa TRC Jamila Mbarouk amesema Walipata taarifa kutoka kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuwa kuna abiria wanafanya udanganyifu huo hivyo TRC imechukua hatua kadhaa ikiwemo kuimarisha ukaguzi wa tiketi.

"Eneo utakalopandia treni utascan tiketi yako,ndani ya treni pia wakaguzi wanafanya ukaguzi wa tiketi pia wakati wa kushuka unatakiwa kuscani ili kubaini kama kuna udanganyifu wowote, kama itakuwa kuna abiria kafanya udanganyifu basi alarm zitapiga kelele hivyo walinzi watakuja kuangalia kuna shida gani".

Ameongeza kuwa Abiria hususani wanaopanda katikati ya safari kuanzia stesheni ya ruvu na ngelengele ndio wengi wanafanya udanganyifu huo ambapo TRC kwa kushirikiana na vyombo vya usalama tayari wamewakamata baadhi ya abiria hao na kuwafikisha Mahakani,Pia katika sakata hilo TRC imewakamata watu kadhaa waliokuwa wanakata tiketi nyingi kwa wakati mmoja na kwenda kufanya udanganyifu.

Aidha ameongeza Kuwa tayari baaadhi ya abiria wanaofanya udanganyifu huo wameshatiwa mbaroni na wengine kufikishwa mahakamani huku wengine wakipiga faini ya kulipa mara mbili zaidi ya nauli waliopaswa kulipa

"tunafanya haya yote kuhakikisha mali ya umma wa Watanzania haipotei hivi hivi kwani ni wajibu wetu wote kulitunza Shirika kwa kulipa nauli stahiki" amesema

Pia soma DOKEZO - Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu

Jamila ameongeza kuwa Kwasasa ili kupanda treni ya SGR ni lazima uwe na kitambulisho chochote kinachoonesha sura ya muhusika na jina lake kamili ambalo pia litafanana na lile ambalo limeandikwa kwenye tiketi yake ili kudhibiti udanganyifu kwani pia kulibainika kuwepo kwa watu ambao walikuwa wakinunua tiketi nyingi ambazo hawakujulikana wanakozipeleka ambao nao tayari wametiwa nguvuni.

Aidha amewataka abiria kuwa waadilifu kwa kulinda mali ya umma na kuhakikisha kila mtu anakuwa mlinzi wa mwenzake kwa kuwafichua wanaohujumu na kusisitiza kuwa kwa yoyote atakayebainika kuhujumu shiriaka atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Source: HABARI 101 TZ Blog
 
Kama wanajua wizi ni kawaida, kwanini wasijipange tangu mwanzo
Kuna technologies za kila aina leo
Yaani baada ya wizi ndio wana scan?
Au kwa kuwa Takukuru wameshtukia mchezo?
 
Nasikia wafuasi wa mbowe wengi pia wanahusika
 
Wekeni picha zao hadharani tuwatambue na tulisaidie shirika kuwamonitor
 
Yaani kila mahali Bongo ni ujanja ujanja tu,na ukifuata utaratibu unaotakiwa eti watu wengine wanakuona mjinga sana! Hata mkiwa kwenye foleni bado watakuja watu wakuleta ujanja ujanja wa kujichomeka mbele!!
Hio ndio Bongo sio kujichomeka tu yule mtoa huduma anaweza akaja kuwachomeka watu wake waliofika muda huo huo na nyinyi mmepanga foleni muda mrefu na akawahudumia na msimfanye kitu hio ndio Bongo
 
Siku moja baada ya taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro kutoa ripoti inayoonyesha kuwepo kwa abiria wenye lengo la kuhujumu Shirika Hilo hatimaye Leo Shirika la Reli (TRC) Limekiri kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu kwa baadhi ya abiria wa Treni ya umeme (SGR) kwa kukata tiketi za kushuka njiani na baadae kupitiliza vituo wanavyopaswa kushuka ikiwa ni nje ya thamani ya fedha zao.

Akizingumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa TRC Jamila Mbarouk amesema Walipata taarifa kutoka kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuwa kuna abiria wanafanya udanganyifu huo hivyo TRC imechukua hatua kadhaa ikiwemo kuimarisha ukaguzi wa tiketi.

"Eneo utakalopandia treni utascan tiketi yako,ndani ya treni pia wakaguzi wanafanya ukaguzi wa tiketi pia wakati wa kushuka unatakiwa kuscani ili kubaini kama kuna udanganyifu wowote, kama itakuwa kuna abiria kafanya udanganyifu basi alarm zitapiga kelele hivyo walinzi watakuja kuangalia kuna shida gani".

Ameongeza kuwa Abiria hususani wanaopanda katikati ya safari kuanzia stesheni ya ruvu na ngelengele ndio wengi wanafanya udanganyifu huo ambapo TRC kwa kushirikiana na vyombo vya usalama tayari wamewakamata baadhi ya abiria hao na kuwafikisha Mahakani,Pia katika sakata hilo TRC imewakamata watu kadhaa waliokuwa wanakata tiketi nyingi kwa wakati mmoja na kwenda kufanya udanganyifu.

Aidha ameongeza Kuwa tayari baaadhi ya abiria wanaofanya udanganyifu huo wameshatiwa mbaroni na wengine kufikishwa mahakamani huku wengine wakipiga faini ya kulipa mara mbili zaidi ya nauli waliopaswa kulipa

"tunafanya haya yote kuhakikisha mali ya umma wa Watanzania haipotei hivi hivi kwani ni wajibu wetu wote kulitunza Shirika kwa kulipa nauli stahiki" amesema

Pia soma DOKEZO - Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu

Jamila ameongeza kuwa Kwasasa ili kupanda treni ya SGR ni lazima uwe na kitambulisho chochote kinachoonesha sura ya muhusika na jina lake kamili ambalo pia litafanana na lile ambalo limeandikwa kwenye tiketi yake ili kudhibiti udanganyifu kwani pia kulibainika kuwepo kwa watu ambao walikuwa wakinunua tiketi nyingi ambazo hawakujulikana wanakozipeleka ambao nao tayari wametiwa nguvuni.

Aidha amewataka abiria kuwa waadilifu kwa kulinda mali ya umma na kuhakikisha kila mtu anakuwa mlinzi wa mwenzake kwa kuwafichua wanaohujumu na kusisitiza kuwa kwa yoyote atakayebainika kuhujumu shiriaka atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Source: HABARI 101 TZ Blog
Matendo yanafanyika ndani ya himaya yenu mnayajua, wale mashosti wenu ndani ya himaya yenu wanafanya kazi gani? Kama hawawezi kujua nani anashuka kituo kifuatacho basi ni bora muwapigie mchiriku wawe wanawaburudisha abiria.
 
Back
Top Bottom