Tanzania Railways Corp
Govt Institution
- Mar 23, 2018
- 292
- 690
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapenda kuuarifu umma kuwa, picha mjongeo (video) inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai Kichwa cha treni ya SGR kikiwa kinatoa mlio usio wa kawaida siyo ya kweli ni uzushi.
Baada ya kufuatilia kwa makini, Shirika linathibitisha kuwa treni zote za SGR zinafanya kazi kwa ufanisi na ziko katika hali salama kabisa, aidha hakuna tukio lolote lililoripotiwa linalohusiana na hitilafu ya aina hiyo kama inavyoonekana kwenye video hiyo.
Aidha, TRC inasisitiza kuwa usalama wa abiria na mali zao ni kipaumbele cha juu, na mifumo yote ya kiuendeshaji wa treni hukaguliwa mara kwa mara na wataalamu ili kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa kwa ubora na usalama wa hali ya juu.
Shirika linawaomba wananchi kupuuza na kutoendelea kusambaza taarifa hizo zisizo sahihi, na badala yake kupata taarifa sahihi kupitia vyanzo rasmi vya TRC.
TRC inaendelea kuwahakikishia Watanzania kuwa huduma za treni ya kisasa ya SGR ni salama, za uhakika, na zinaendelea kuboreshwa kila wakati kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.