Tanzania Railways Corp
Govt Institution
- Mar 23, 2018
- 292
- 690
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linawaarifu wananchi na abiria wote kuwa, kumekuwepo na vitambulisho mbalimbali vilivyoachwa katika treni na stesheni za SGR na MGR kutokana na sababu tofauti wakati wa safari.
Vitambulisho hivyo ni pamoja na: kitambulisho cha taifa (NIDA), leseni za udereva, vitambulisho vya mpiga kura, pamoja na nyaraka nyingine muhimu za utambulisho.
Kutokana na hali hiyo, TRC inawaomba wananchi wote wanaodhani wamepoteza au kuacha vitambulisho vyao kufika katika stesheni za TRC zilizo karibu nao ili kuvichukua.
Zoezi la urejeshaji wa vitambulisho hivyo litafanyika kwa miezi mitatu, kuanzia Aprili 15, 2026 hadi Julai 15, 2026 katika stesheni zote za TRC zinazohusika.
Baada ya kukamilika kwa muda huo, vitambulisho vyote ambavyo havitakuwa vimechukuliwa vitarejeshwa kwa mamlaka husika kwa hatua zaidi.
TRC inasihi ushirikiano katika zoezi hili kwa wahusika kufika kuchukua nyaraka zao ndani ya muda uliopangwa.