TRC yalipa Tsh. Milioni 565.4 fidia kwa Wananchi wa Nyamori

TRC yalipa Tsh. Milioni 565.4 fidia kwa Wananchi wa Nyamori

Tanzania Railways Corp

Govt Institution
Joined
Mar 23, 2018
Posts
292
Reaction score
690
Shirika la Reli Tanzania (TRC), linaendelea na zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita Tabora–Kigoma, ambapo Julai 15, 2026 Wananchi wa Kijiji cha Nyamori kata ya ya Simbo Halmashauri ya Kigoma, wameanza kupokea stahiki zao.

Jumla ya shilingi milioni 565.4 zimelipwa kwa wanufaika 198, ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Ardhi na Sheria ya Utwaaji Ardhi zinazotaka fidia kulipwa ndani ya muda uliowekwa, ili kuwawezesha wananchi kurejesha mali zilizotwaliwa kwa ajili ya kupisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya SGR.

 
Back
Top Bottom