Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Dar es Salaam, Tarehe 2 Agosti 2024
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kwa abiria waliosafiri kutoka Dodoma saa 2.15 usiku kuelekea Dar es Salaam Agosti 1, 2024 kwa treni ya mwendo kasi kuchelewa kuwasili kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea eneo la Mtaa wa Mshikamano Kata ya Kihonda mkoani Morogoro.
Hitilafu za kiufundi zilitokea majira ya saa 4.33 usiku na kushughulikiwa kwa muda wa takriban saa moja na kusababisha treni hiyo ya abiria kutoka Dodoma kuchelewa kuwasili Dar es Salaam kwa wakati uliopangwa.
Shirika la Reli Tanzania linatoa taarifa kuwa treni ya abiria iliyobeba viongozi na wananchi wengine waliotoka Dodoma saa 1 usiku baada ya kushiriki sherehe za uzinduzi wa SGR waliwasili Dar es Salaam kwa muda uliopangwa bila hitilafu yeyote.
TRC inazingatia usalama wa abiria kabla na wakati wa safari ili kuepusha madhara kwa watumiaji wa huduma za usafiri wa reli na linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Jamila Mbarouk
MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO