TRC yaomba radhi kutokana na hitilafu ya umeme katika Treni ya SGR

TAARIFA KWA UMMA HITILAFU YA TRENI YA KAWAIDA YA ABIRIA KUTOKA DODOMA KUELEKEA DAR ES SALAAM

Dar es Salaam, Tarehe 2 Agosti 2024

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kwa abiria waliosafiri kutoka Dodoma saa 2.15 usiku kuelekea Dar es Salaam Agosti 1, 2024 kwa treni ya mwendo kasi kuchelewa kuwasili kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea eneo la Mtaa wa Mshikamano Kata ya Kihonda mkoani Morogoro.

Hitilafu za kiufundi zilitokea majira ya saa 4.33 usiku na kushughulikiwa kwa muda wa takriban saa moja na kusababisha treni hiyo ya abiria kutoka Dodoma kuchelewa kuwasili Dar es Salaam kwa wakati uliopangwa.

Shirika la Reli Tanzania linatoa taarifa kuwa treni ya abiria iliyobeba viongozi na wananchi wengine waliotoka Dodoma saa 1 usiku baada ya kushiriki sherehe za uzinduzi wa SGR waliwasili Dar es Salaam kwa muda uliopangwa bila hitilafu yeyote.

TRC inazingatia usalama wa abiria kabla na wakati wa safari ili kuepusha madhara kwa watumiaji wa huduma za usafiri wa reli na linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Jamila Mbarouk
MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
Mwendokasi imewashinda ukija atcl imewashida hiyo SGR nayo imewashinda wanachowezaxni uffisadi tu
 
Watachokaa mbonaaa waulize mwendokasiii walijidai kuanza na mtoto kama hawaa siku hiziii sasa kama wanapakia mbuzii..!!
 
Tunaomba majibu juu ya power bank za treni au wametutapeli wameleta ambazo hazina mfumo huo?
Ikiwa ndivyo wahusika wachukuliwe hatua kali.
Ni kweli walisema zina power bank,any way Kuna haja ya kuwa na vichwa vingine toka Sweden,kama mtu alitenegeza scania hawezi shindwa jambo dogo kama Hilo,naomba tafadhali mtulinde kwa hili.
 
Hii

comment yako izingatiwe, ikiwezekana Iwekiwe Lamination
 
TAARIFA KWA UMMA HITILAFU YA TRENI YA KAWAIDA YA ABIRIA KUTOKA DODOMA KUELEKEA DAR ES SALAAM

Dar es Salaam, Tarehe 2 Agosti 2024

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kwa abiria waliosafiri kutoka Dodoma saa 2.15 usiku kuelekea Dar es Salaam Agosti 1, 2024 kwa treni ya mwendo kasi kuchelewa kuwasili kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea eneo la Mtaa wa Mshikamano Kata ya Kihonda mkoani Morogoro.

Hitilafu za kiufundi zilitokea majira ya saa 4.33 usiku na kushughulikiwa kwa muda wa takriban saa moja na kusababisha treni hiyo ya abiria kutoka Dodoma kuchelewa kuwasili Dar es Salaam kwa wakati uliopangwa.

Shirika la Reli Tanzania linatoa taarifa kuwa treni ya abiria iliyobeba viongozi na wananchi wengine waliotoka Dodoma saa 1 usiku baada ya kushiriki sherehe za uzinduzi wa SGR waliwasili Dar es Salaam kwa muda uliopangwa bila hitilafu yeyote.

TRC inazingatia usalama wa abiria kabla na wakati wa safari ili kuepusha madhara kwa watumiaji wa huduma za usafiri wa reli na linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Jamila Mbarouk
MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
Shida tulio jenga reli mmetutupa pembeni wamewekwa walio soma kwa madigrii wakati sisi la saba, nne, tatu na lapili mmetuacha pembeni wakati sisi ndiyo tuna jua kwa kina chamgamoto za huu mradi
 
Back
Top Bottom