TRC yaomba radhi Treni ya Mchongoko Dar-Dodoma kusimama ghafla kati ya Pugu na Soga

TRC yaomba radhi Treni ya Mchongoko Dar-Dodoma kusimama ghafla kati ya Pugu na Soga

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

trc.jpg

Taarifa kwa umma,

Shirika la reli tanzania (trc) linaomba radhi kwa abiria wa treni ya mchongoko (emu) walioanza safari yao dar es salaam kwenda dodoma saa 2:00 asubuhi na kusimama ghafla majira ya saa 2:20 kati ya pugu na soga.

Aidha, tunaomba radhi pia kwa abiria wetu wa treni ya saa 11:15 alfajiri kutoka dodoma na treni ya saa 3:30 kutoka dar es salaam ikijumuisha safari nyingine za siku ya leo ambazo zimeathiriwa kufuatia hitilafu kwenye mifumo yetu ya uendeshaji

Mafundi wetu wako eneo la tukio wanafanyia kazi changamoto hiyo, tutaendelea kuwapatia taarifa

Tunatanguliza shukurani.

Pia soma: KERO - √ - Treni ya mchongoko Dar-Dodoma imeharibika porini toka saa 2 asubuhi kati ya eneo la Pugu na Soga
 
litawatoeni roho wote yaani, poleni sana walioharibu ratiba zao za kazi na interview..poleni kwa hasara hiyo
 
Wakuu,

Taarifa kwa umma,

Shirika la reli tanzania (trc) linaomba radhi kwa abiria wa treni ya mchongoko (emu) walioanza safari yao dar es salaam kwenda dodoma saa 2:00 asubuhi na kusimama ghafla majira ya saa 2:20 kati ya pugu na soga.

Aidha, tunaomba radhi pia kwa abiria wetu wa treni ya saa 11:15 alfajiri kutoka dodoma na treni ya saa 3:30 kutoka dar es salaam ikijumuisha safari nyingine za siku ya leo ambazo zimeathiriwa kufuatia hitilafu kwenye mifumo yetu ya uendeshaji

Mafundi wetu wako eneo la tukio wanafanyia kazi changamoto hiyo, tutaendelea kuwapatia taarifa

Tunatanguliza shukurani.

Pia soma: TRC yaomba radhi Treni ya Mchongoko Dar-Dodoma kusimama ghafla kati ya Pugu na Soga
Kazi wanayoweza TRC ni kuomba radhi kwa wakati
 
hilo dude ipo siku litaondoko na roho za watu ni swala la muda
Punguza Roho ya kichawi wewe.
Mlisema hivyo hivyo wakati Magufuli anazindua Ndege na mkawa mnaombea mabaya kila uchao lkn mpaka sasa miaka 7 hakuna ndege ya Air Tanzania iliyowahi kugonga hata mbuzi.

Maneno yako ya Kishetani yakupate wewe na familia yako, Watanzania wengine kwa Uwezo wa Mungu watabaki salama. Ameeen
 
Wameomba radhi mbona hawajasema tatizo ni nini?

CCM sio lazima miaka nenda Rudi muongoze nyinyi nchi embu waachieni na wengine wawekeze akili zao kuendesha hii nchi maana imewashinda
 
Wameomba radhi mbona hawajasema tatizo ni nini?

CCM sio lazima miaka nenda Rudi muongoze nyinyi nchi embu waachieni na wengine wawekeze akili zao kuendesha hii nchi maana imewashinda
Waachie kazi hii vyombo mbalimbali wachunguze unadhani mradi kama huu utapendwa na maadui zetu??
 
Back
Top Bottom