Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Eneo hili miaka yote huwa namijusi na vyura wengi sana wanaosababisha magurudumu yateleze.Wakuu,
Taarifa kwa umma,
Shirika la reli tanzania (trc) linaomba radhi kwa abiria wa treni ya mchongoko (emu) walioanza safari yao dar es salaam kwenda dodoma saa 2:00 asubuhi na kusimama ghafla majira ya saa 2:20 kati ya pugu na soga.
Aidha, tunaomba radhi pia kwa abiria wetu wa treni ya saa 11:15 alfajiri kutoka dodoma na treni ya saa 3:30 kutoka dar es salaam ikijumuisha safari nyingine za siku ya leo ambazo zimeathiriwa kufuatia hitilafu kwenye mifumo yetu ya uendeshaji
Mafundi wetu wako eneo la tukio wanafanyia kazi changamoto hiyo, tutaendelea kuwapatia taarifa
Tunatanguliza shukurani.
Pia soma: TRC yaomba radhi Treni ya Mchongoko Dar-Dodoma kusimama ghafla kati ya Pugu na Soga