Shirika la Reli Tanzania, TRC linawatangazia watu wote kuwa safari za treni la biria kutoka Dar kuelekea Moshi zitarejea rasmi mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka 2019
Nauli Dar - Moshi inategemewa kuwa ifuatavyo:
- Daraja la tatu Tsh. 16,500
- Daraja la pili kukaa Tsh. 23,500
- Daraja la pili kulala Tsh. 39,100
================================
Dar es Salaam. Ikiwa tunaelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019, abiria wa Kanda ya Kaskazini watakuwa na kicheko kwao baada ya treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi itaanza Desemba.
Tayari Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa tangazo la kuanza kwa usafiri huo na kuthibitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaac Kamwele.
Waziri Kamwele amesema kama Serikali imefurahi kufikia hatua hiyo ukizingatia treni hiyo ilikuwa ianze tangu Septemba 2019.
Hata hivyo, amesema kutokana na changamoto za kunyesha mvua na kusababisha baadhi ya miundombinu ikiwemo ya reli kuharibika katika ukanda huo wa Kaskazini ndio maana kukawepo na uchelewaji wa kuanza kwake.
“Sasa ile tabia ya wafanyabiashara pale stendi ya ubungo kulangua abiria tiketi wakati watu wakienda kula sikukuu na ndugu zao itakoma, kwani hata mimi ilishanikuta na kama Serikali tulikuwa tunahangaika kutafuta njia ya kukomesha vitendo hivyo na ujio wa treni hii ya abiria utasaidia,” amesema
Kuhusu nauli, Waziri Kamwele amesema wameacha ileile iliyokuwa ikitumiwa tangu kusitishwa kwa usafiri huo na ndio maana hawakuitisha hata kikao cha wadau kuhitaji maoni ya nauli.
Wakati kuhusu uwezo wa kusafirisha abiria, amesema itategemea na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) itakavyowapangia japokuwa uwezo wa behewa moja ni kubeba abiria 80 huku kichwa kimoja cha treni kikiwa na uwezo wa kubeba mabehewa 20.
“Katika idadi ya abiria tutakaobeba tutasubiri Latra watuambie kwa kuwa wenyewe ndiyo wataalam wa usafiri lakini uwezo wetu kwa behewa moja ni kubeba abiria 80 huku kichwa kikiwa na nguvu ya kubeba mabehewa 20,”amesema.
Treni hiyo itakayopita Korogwe mkoani Tanga, TRC imetangaza nauli zake ambapo Dar es Salaam hadi Korogwe daraja la tatu itakuwa Sh10,700, daraja la pili kukaa Sh15,300 na daraja la pili kulala Sh25,400.
Wakati kwa abiria watakaotoka Dar es Salaam kwenda Moshi daraja la tatu itakuwa Sh16,500, daraja la pili kukaa Sh23,500 na daraja la pili kulala Sh39,100.
Okee safi sana wametime muda muafaka mana mwezi December nauli zamabasi zinapanda sana na usafiri unakua washida mno kwaiyo natumai ndugu zangu wa uchagani utatuzi umepatikana
Tutakoga mbege mpaka utosi uanze kudunda kama wa mtoto mchanga. Huku ndio kwa kuelekeza hela zetu, sio kununua ndege za kwenda Katavi wakati wenyewe wana ndege zao.
Wameweka mabehewa ya aina gani?
Je safari itatumia masaa mangapi?
HAWA JAMAA ZETU HUWA WANAJALI SANA UBORA,SIO SAWA NA WALE WANAOSAFIRI NA MAJIKO YAO NA KUANZA KUPIKIA HUMO HUMO.
Pilikapilika za watu kwenda X-Mas na Mwaka Mpya zinakaribia kuanza, kwa wale tunaokwenda njia ya Moshi-Arusha tunajiandaa kwa maumivu ya nauli kubwa ya mabasi na ukosefu wa usafiri wa kuelekea njia hiyo.
Ombi kwa shirika la reli nchini, kama reli ya Dar - Moshi iko sawa tunaomba tupatiwe usafiri wa mabehewa ya treni kwenda njia hiyo ya kuelekea Arusha na vituo vyake mbalimbali.
Hii itasaidia:
- kupata usafiri kwa watu wengi
- Kushusha bei ya nauli za mabasi ya wafanyabiashara wa njia hiyo nyakati hizi za mwaka
- TRC itaongeza mapato yake
- Serikali itaongeza wigo wa mapato.
- Itaboresha utalii wa ndani
- Itapunguza ajali za barabarani kwa njia hii katika kipindi hiki
Hahaa kwamba wanataka waanze kuoanisha speed yahiyo treni na speed ya KILIMANJARO COACH ..
Hahaa duh najikuta nacheka sana hapa nikikumbuka ile kauli ya mkulu aliyosema kama unataka speed kapande ndege ya jeshi