TRC yatangaza Tenda ya Kusambaza, Kufunga na Kuboresha Mfumo wa Kamera za Ulinzi (CCTV) kwenye mabehewa ya abiria ya SGR

TRC yatangaza Tenda ya Kusambaza, Kufunga na Kuboresha Mfumo wa Kamera za Ulinzi (CCTV) kwenye mabehewa ya abiria ya SGR

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza Tenda ya Kusambaza, Kufunga, na Kuboresha Mfumo wa Kamera za Ulinzi (CCTV) kwenye mabehewa ya abiria ya Reli ya Kisasa (SGR).

Tenda hiyo inahusisha;
  • Kusambaza kamera maalum za reli (4 MP IP CCTV), mifumo ya kurekodi picha (8-Channel NVRs), na vifaa vya kuhifadhia kumbukumbu (Storage Devices).
  • Kufunga mifumo yote ya nyaya na mabano (brackets/cabling) pamoja na kompyuta za uchunguzi wa picha (Workstations) na vifaa vya kubeba vya matengenezo (Portable Terminals).
  • Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 30 wa TRC na kusambaza vipuri (Spare Parts).
Deadline ni tarehe 19/08/2026 saa 8:00 Mchana (2:00 PM) kwa saa za Tanzania. Taarifa zaidi imeambatishwa hapo chini.

Screenshot 2026-08-13 174045.png

Mdau alivyoambiwa kamera za SGR ni mapambo baada ya kuibiwa laptop yake....
Majuzi kuna mdau humu alileta kero yake akionyesha wasiwasi wake mkubwa baada ya kuibiwa laptop katika moja ya mabehewa ya SGR, na aliporipoti aliambiwa kamera hizo hazifanyi kazi, ni mapambo tu, yamekaa kutisha watu ila kikikuramba hakuna usaidizi utapata. Jambo hili liliwapa wengi maswali na kuwaongezea wasiwasi, vipi kama likitokea jambo kubwa na kusababisha athari kubwa? Ina maana hakutakuwa na msaada wowote na waliofanya tukio wataendelea na maisha yao kama kawaida kutokana na kuwa hakuna kithibitisho.

Pia soma Nimeibiwa Laptop kwenye Treni ya SGR, wameniambia CCTV za kwenye behewa ni urembo tu, hazifanyi kazi!

TRC walitolea ufafanuzi - ulinzi upo wa kutosha, kamera zinafanyakazi vizuri....
TRC hawakupitisha muda wakatoa ufafanuzi na kuwaondoa wasiwasi wananchi kuwa ulinzi upo wa kutosha na kwamba kamera zote zinafanyakazi vizuri. Suala hili likazua mjadala mtandaoni - kama kamera zote zinafanyakazi, basi waonyeshe kile kilichotokea, ili wamkamate muhusika na kumrudishia laptop yake hata kama mdau alisema alishanunua nyingine.

Pia soma Kuhusu kamera za SGR kutofanya kazi, TRC wawaondoa wasiwasi wananchi, wasema zinafanya kazi!

Video ya Content Creator ilivyoibuka na kuelezea namna alivyosahau begi lenye laptop kwenye SGR na kuvipata....
Baada ya ufafanuzi kutoka mtengeneza maudhui mtandaoni (Content Creator) akapost video jinsi alivyosahau begi lake lenye laptop na vitu vingine, na kwenda SGR wakasema wanafutilia mpaka wakalipata na wakampatia na begi lake likiwa na kila kitu na kusema kuanzia hapo amewaamini sana na hataacha kutumia SGR na :BearLaugh::KEKWlaugh:@Tanzania Railways Corp mnatuona sisi ma😒ko yenu eeeeh? Hizo hela mmepa jamaa afagie your mess si hata mngempa jamaa ikachangia kwenye gharama za kununua laptop mpya?


Halafu baada ya show yao hao wameenda kutangaza tenda ya kusambaza, kufunga na kuboresha mifumo ya CCTV! Uwajibikaji na taasisi za Tanzania kama ilivyokuwa serikali yake ni hivi🫲🫱

Haya wa wenye mna vigezo mwende mkaombe huko watu tusije tukapoteza vya thamani zaidi au akaingia 'gaidi' wakashindwa kumwona😂
 

Attachments

  • Screenshot 2026-08-13 174217.png
    Screenshot 2026-08-13 174217.png
    81.1 KB · Views: 9
  • Screenshot 2026-08-13 174235.png
    Screenshot 2026-08-13 174235.png
    54.7 KB · Views: 10
  • tenda trc.pdf
    tenda trc.pdf
    1.2 MB · Views: 8
Back
Top Bottom