Treasure bond and bill: Naomba kueleweshwa maana ya hizi financial terms

jembelamkono

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
2,733
Reaction score
2,012
Habari wanajukwaa?
Kwa kutumia mifano iliyowahi kutangazwa hapa nchini,naomba kueleweshwa maana ya hizi financial terms na mifano ya jinsi zinavyo fanyika kwa hapa nchini kwetu.
Msaada wenu wajuzi wa hizi mambo.
 
Kwanza sio financial terms. Zinaitwa Financial Instruments.
Pia zio tresure bill bali Treasury Bills na Government bonds.
Treasury bills hizi ni dhamana zinazotumika pale serikali inapokopa mkopo usio zidi mwaka mmoja.
Govt bonds ni dhamana inayotolewa na serikali inapokopa mkopo wa muda mrefu unaozidi mwaka mmoja.
Dhamana hii huwa katika mfumo wa hati / certificate.
Kwa hiyo tofauti kubwa iko kwenye maturities au muda wa kuiva. Bills huiva chini ya mwaka wakati bonds zinachukua zaidi ya mwaka kuiva.
 
Unaweza kutolea mfano ambao serikali imeuza/kutangaza kwa miaka ya karibuni?
Na je watu waliokopesha wanaweza kufaidika kwa kwa faida kiasi gani?
 
Basically zinakuwa issued na Govt kupitia BOT. Faida inapatikana kwa sababu zinakua issued at discount. Maana yake unaweza ukanunua(hiyo certificate) kwa maana ya kuikopesha serikali at 97 halafu muda wa maturity unapofika serikali inakulipa at 100. So the difference ndio faida yako sasa itategemea umenunua za kiasi gani. Faida yake ni guaranteed, they are termed to be risk free instruments kwamba ni lazima serikali italipa.
Hizi huwa zinauzwa na benki kuu na zinatangazwa kwenye magazeti.
 
Kwanza sio financial terms. Zinaitwa Financial Instruments.
Pia zio tresure bill bali Treasury Bills na Government bonds.
Treasury bills hizi ni dhamana zinazotumika pale serikali inapokopa mkopo usio zidi mwaka mmoja.
Govt bonds ni dhamana inayotolewa na serikali inapokopa mkopo wa muda mrefu unaozidi mwaka mmoja.
Dhamana hii huwa katika mfumo wa hati / certificate.
Kwa hiyo tofauti kubwa iko kwenye maturities au muda wa kuiva. Bills huiva chini ya mwaka wakati bonds zinachukua zaidi ya mwaka kuiva.
Dadavua zaidi.Kuiva ni kufikia ule mda wa makubaliano au nini?
 
Post kama hizi zinatoa shule tosha,
Majibu yanayotolewa humu watu tuliyasomea kwa mamillion ya pesa,
Leo hii watu wanayapata kwa mb za jero
Faida hizi rais wenu hazijui analeta figusufigisu kufungia mitandao,
Stupid Tanzania
 
Ile tarehe ya kuiva itakuwa kwa hiyo karatasi hivyo ikifika unakuta mkwanja wako. Ni kama unavyoweka fixed deposits ikifika muda wake unachukua pesa na riba au unaamua kuirejesha tena kwa mkataba mpya. Ukitaka zaidi Ingia Google utapata details na mfano japo miingi ya nchi za nje.
 
Hivi benki na mtu binafsi wote wanaruhusiwa kununu hizi? Zinauzwa kupitia wapi, soko la hisa, mabenki au BOT kwenyewe?
 
zinakuwa na faida kiasi chake pia inategemea umenunua za kiasi gani kadri unavyokuwa na nyingi ndivyo unakuwa na faida nyingi pindi zinapo mature, ukiingia katika soko la hisa la dar es salaam utakuta kule wanatangaza mara kwa mara pia hata BOT huwa wanatangaza, na kwenyemagazeti, watu wenye fedha nyingi ndio wanapata faida sana katika hii mambo maana hata baadhi ya bank hununua hati na baadae hijipatia faida nzuri. ni ka vile fixed a/c ila hizi zinafaida zaidi japo si ka faida ya biashara za moja kwa moja.
 
Post kama hizi zinatoa shule tosha,
Majibu yanayotolewa humu watu tuliyasomea kwa mamillion ya pesa,
Leo hii watu wanayapata kwa mb za jero
Faida hizi rais wenu hazijui analeta figusufigisu kufungia mitandao,
Stupid Tanzania
Maneno kuntu
 
Back
Top Bottom