Mitazamo ya uzuri wa mwanamke siyo ya kudumu, inabadilika kulingana na nyakati.
Enzi za mabibi zetu wanawake wenye mwanya walionekana kuwa ndiyo warembo zaidi. Ikawalazimu bibi zetu kubomoa meno ya mbele ili kupata pengo litakalohesabika kama mwanya.
Enzi za mama zetu, wanawake wenye rangi ya mtume walionekana kuwa ndiyo wenye soko kubwa sana kwa wanaume. Ikawalazimu mama zetu kujichubua kwa kutumia mkorogo ili kuondoa rangi nyeusi waweze kuonekana weupe.
Katika enzi hizi, mwanamke mwenye chura anamiliki dunia yote. Akivaa nguo ikayaonesha vema makalio, basi kila atakapopita atatazamwa. Hii inawalazimu akina dada kuvaa vigodoro ili kuongeza ukubwa wa vikalio vyao asilia. Na wengine hupaka mafuta maalumu ya kukuza makalio maarufu kama "machina".
Na tunakoelekea "kiuno nyigu" ndiyo inaenda kuchukua nafasi ya makalio makubwa. Naona trend ya wadada kubana tumbo inakuja kwa kasi sana.