Tanzania Railways Corp
JF-Expert Member
- Mar 23, 2018
- 251
- 595
Seti ya kwanza ya EMU
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa ya kuwasili katika Bandari ya Dar es salaam kwa seti ya kwanza ya Treni ya kisasa ya EMU, Vichwa vitano vya umeme na Mabehewa matatu ya Abiria ( iliyowasili ni seti moja ambayo kikawaida hufungwa behewa nane na vichwa viwili kimoja mbele na kimoja nyuma).
Taarifa iliyotolewa leo April 03,2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano- TRC, Jamila Mbarouk imeeleza yafuatayo ——— > “Kupitia TRC ilifanya manunuzi ya seti kumi (10) za Treni za kisasa zijulikanazo kama Electric Multiple Unit (EMU) kutoka kwa Watengenezaji kampuni ya Hyundai Rotem ya Korea Kusini, seti moja ya EMU ina uwezo wa kubeba Abiria 589 na kutembea kilomita 160 kwa saa, EMU ni treni iliyoundwa kwa teknolojia ya kisasa inayomuwezesha Abiria kupata huduma kama Wi-FI, sehemu za kukaa Watu wenye mahitaji maalum n.k”
“Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania imepokea jumla ya Mabehewa 65 ya Abiria, Vichwa 9 vya umeme na seti moja ya EMU, seti nyingine za EMU zitaendelea kuwasili kila mwezi hadi Oktoba 2024, kuwasili kwa vitendea kazi kunaifanya TRC kuwa tayari kuanza huduma za usafirishaji Abiria katika reli ya kiwango cha kimataifa”
“Maendeleo ya mradi wa SGR awamu ya kwanza yamefikia asilimia 98.90 kwa kipande cha Dar es salaam - Morogoro (KM 300), asilimia 96.51 kipande cha Morogoro - Makutupora, asilimia 13.98 kipande cha Makutupora - Tabora, asilimia 5.44 kipande cha Tabora - Isaka, asilimia 54.01 kipande cha Mwanza - Isaka