KERO Treni ya mchongoko Dar-Dodoma imeharibika porini toka saa 2 asubuhi kati ya eneo la Pugu na Soga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Jamaa yangu yumo humo anasema wameambiwa wanaanza safari sio mida mrefu
Hawajasema wataanza safari "sio muda mrefu.'

Wamesema ndani ya saa moja!

Itakuwa mida ya saa nane!

Treni limebuma saa mbili asubuhi. Itakuwa limebuma masaa sita.

Treni la Gongo La Mboto halijawahi kugoma masaa 6. In fact, halijawahi kugoma, for all we know!

Hili jipya, la kisasa, la kitaifa, kwa nini likate moto porini masaa sita ???
 
Chombo kikiwa kipya means kuna mifumo bado inajaribiwa, itakaa sawa tu
 
Marekebisho ya kiufundi ?

Kifaa kipya!

Ufundi wa nini ???

Niliishi Brooklyn, New York. Subway lao limejengwa mwaka wa 1904.

Sijawahi kuona limekata moto.

La kwetu lina miezi miwili unusu. Kila siku linakata moto porini.

Tatizo nini ????
hakuna haja ya kubabaika gentleman

Taarifa ya mamlaka ya uendeshaji iko clear sana na wenye haraka wako huru wanaweza kutumia usafiri mbadala. Lakini haiwekezani kulazimisha kitu kilicho nje ya uwezo wa kibinadamu halafu kisababishe au kuleta madhara kwa jamii 🐒
 
Kama sio bikra usioe
 
sasa si wawape kampuni binafsi tu waendeshe hilo tren wao wabakie kuratibu na kusimami tu..
tuna upumbavu mwiiiingiiii kupitiliza!
 
Mungu azidi kuniweka, maana ningepitwa na mengi sana aiseeee...🤨
 
Kuna kama hujma ktk hili viongozi wafatilie hili
 
Haya wenye mabasi fursa hiyo ,mkafaulishe sasa
 
Umeweka msisitizo kwenye errors lakini huku kwetu ni human errors kwa kiasi kikubwa.
 
Tunalishughulikia Wataondoka Tu
Buses Zinachukua Point 3
Mbona hata ma bus nayo huwa yanapata break down, vyombo vya moto kupata breakdown ni jambo la kawaida sana, kama wwe vile binaadamu kuumwa ni jambo la kawaida sana! Kanaumwa katoto kachanga ambako ndiyo binaadamu mpya huyo,itakua sembuse kitu cha mchongokoo!!
 
Siasa imeingia hadi kwenye vyombo vya usafiri ni shida tupu.
 
Si vituoni, huko maporini.

Single track ndiyo inaweza kusababisha ajali zaidi, sasa kwa nini unasema single track ajali itakuwa na ngedere tu?
Sawa nimekuelewa. Ukichosema kinaweza kabisa kutokea.

Uzembe katika traffic management, poor maintenance na weak technical know-how ya mifumo ya electronic ni mambo ya kutarajiwa sana kwa watu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…