Imetoka Dodoma saa 12 kamili asubuhi.
Tangu saa mbili asubuhi, treni imekwama. Sasa inaenda saa 7 mchana, na hakuna matumaini ya kuendelea.
Treni iko kilomita 45 kutoka Dar, porini. Wengine wanashuka na kupanda boda; wanaenda wapi, sijui. Tangazo la TRC linasema mafundi wapo kazini.
Chombo ni kipya, mitambo ya umeme ni mipya, na umeme upo. Nadhani juzi TANESCO walisema tunakimbia na ziada, na maji pia, kama ilivyosemwa na DAWASCO siku tatu zilizopita. Lakini leo, Jumapili, maji yamekata!
Abiria wapo, hivyo operesheni na mtaji wa matengenezo vipo.
Tatizo nini?
Wazalendo ndani ya TRC, tafadhali tujulishe kupitia njia zetu za kujuzana. Viongozi watatudanganya. Hawana dini. Waliwahi kusema Rais ametingwa na kazi Ikulu, kumbe ameshanyooka. Na waliongelea msikitini. Astakafullulilah Ladhim.
****
TAARIFA KUTOKA SHIRIKA LA RELI TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC) LINAOMBA RADHI KWA ABIRIA WA TRENI YA MCHONGOKO (EMU) WALIOANZA SAFARI YAO DAR ES SALAAM KWENDA DODOMA SAA 2:00 ASUBUHI NA KUSIMAMA GHAFLA MAJIRA YA SAA 2:20 KATI YA PUGU NA SOGA
AIDHA, TUNAOMBA RADHI PIA KWA ABIRIA WETU WA TRENI YA SAA 11:15 ALFAJIRI KUTOKA DODOMA NA TRENI YA SAA 3:30 KUTOKA DAR ES SALAAM IKIJUMUISHA SAFARI NYINGINE ZA SIKU YA LEO AMBAZO ZIMEATHIRIWA KUFUATIA HITILAFU KWENYE MIFUMO YETU YA UENDESHAJI
MAFUNDI WETU WAKO ENEO LA TUKIO WANAFANYIA ΚΑΖΙ CHANGAMOTO HIYO, TUTAENDELEA KUWAPATIA TAARIFA
TUNATANGULIZA SHUKURANI
View attachment 3142521