KERO Treni ya mchongoko Dar-Dodoma imeharibika porini toka saa 2 asubuhi kati ya eneo la Pugu na Soga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Shida ni treni jipya limekwama porini.

Kwa nini mitambo mipya inaharibika haribika ovyo ?

Limekuwa gari la mkaa ?

Hata lori la mkaa halikati moto porini likiwa jipya.

Tulinunua mitambo chakavu ? Kwa nini ma VX yao mapya hayakati moto porini ?
Nani alikuwambia trend ni jipya
 
Kama treni ni hovyo na mafundi watakuwa kama treni Yao na mkurugenzi wao
 
kama migahawa ya vyakula vya humo kwenye treni hawauzi vyakula kwa sababu ya treni kufika haraka safari yao, basi siombaya ikihalibika polini ili nao wapate riziki.
 
Treni limepona, limeondoka Soga 10 minutes ago.

Hii ni 11 jioni. Limebuma masaa 9, toka 2 asubuhi.

Magari ya mkaa yaliyogoma saa mbili asubuhi yalishaletewa spea kitambo, yameondoka, na yamesha deliver mikaa.

Waliposema itaondoka in one hour ilikuwa saa 7, some 4 hours ago. Walisema uongo!

Sishangai kuongopewa. Kuna siku walisema Rais hajambo kumbe kafa.
 
Serikali haisaidii wasafiri au raia, inatimiza wajibu wake kwa kutumia kodi za raia kufanya biashara ya usafiri.
 
Treni sio sawa na bus.
 
Acha mawazo hasi mkuu....Wanawasiliana mara nyingi pale Gwara aliembele anamsubiri mwenzake apite kwanza
Haya si mawazo hasi, ni mawazo ya uhalisia. Watu kila siku chache treni linabuma, kwa nini kufikiri kuwa inawezekana siku treni zikagongana iwe ni mawazo hasi?
 
Wabongo tumejaa lawama sana;

Usafirishaji sio kitu perfect; inatokea kwenye Meli, kwenye ndege, kwenye mabasi n.k. Flights zinakuwa rescheduled kwa sababu mbali mbali mara kwa mara na maisha yanaendelea.

Nadhani Ingekuwa treni sio mali ya serikali wala usingelaumu. Shida ni kuwa ni ya serikali na waafrika wengi hawazipendi serikali zao.
 
Mkuu jikite kwenye hoja nini shida!!

Maana umeongea vitu vingi kwa wakati mmoja tukujibu kipi sasa,

Kilichokwamisha safari yako ni hiyo SGR lakini ni kama una mambo mengi kichwani, lawama ni nyingi kuliko kilichokukwamisha.
Kitu ambacho sijawahi kukielewa ni hii treni kuiita SGR ,ambayo ni kirefu cha Standard Gauge Rail... yaani hata media unasikia treni ya SGR yapata changamoto, really??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…