Verrazanno
JF-Expert Member
- Sep 15, 2021
- 454
- 1,011
Imetoka Dodoma saa 12 kamili asubuhi.
Tangu saa mbili asubuhi, treni imekwama. Sasa inaenda saa 7 mchana, na hakuna matumaini ya kuendelea.
Treni iko kilomita 45 kutoka Dar, porini. Wengine wanashuka na kupanda boda; wanaenda wapi, sijui. Tangazo la TRC linasema mafundi wapo kazini.
Chombo ni kipya, mitambo ya umeme ni mipya, na umeme upo. Nadhani juzi TANESCO walisema tunakimbia na ziada, na maji pia, kama ilivyosemwa na DAWASCO siku tatu zilizopita. Lakini leo, Jumapili, maji yamekata!
Abiria wapo, hivyo operesheni na mtaji wa matengenezo vipo.
Tatizo nini?
Wazalendo ndani ya TRC, tafadhali tujulishe kupitia njia zetu za kujuzana. Viongozi watatudanganya. Hawana dini. Waliwahi kusema Rais ametingwa na kazi Ikulu, kumbe ameshanyooka. Na waliongelea msikitini. Astakafullulilah Ladhim.
=====

Ufafanuzi wa TRC soma hapa: TRC yaomba radhi Treni ya Mchongoko Dar-Dodoma kusimama ghafla kati ya Pugu na Soga