KERO Treni ya mchongoko Dar-Dodoma imeharibika porini toka saa 2 asubuhi kati ya eneo la Pugu na Soga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mungu ajaalie "mifumo ya uendeshaji" ndege zetu isitokee.

Watanzania ni bogus sana, utakuta maereva waliamka na pombe, wa kichwa cha mbele anaenda Dodoma wa kichwa cha nyuma anaenda Dar.

Hakuna cha "hitilafu" wala nini kwenye mifumo ya uendeshaji, ni uzembe tu.
 
Imetoka Dodoma saa 12 kamili asubuhi.

Tangu saa mbili asubuhi, treni imekwama. Sasa inaenda saa 7 mchana, na hakuna matumaini ya kuendelea.

Treni iko kilomita 45 kutoka Dar, porini. Wengine wanashuka na kupanda boda; wanaenda wapi, sijui. Tangazo la TRC linasema mafundi wapo kazini.

Chombo ni kipya, mitambo ya umeme ni mipya, na umeme upo. Nadhani juzi TANESCO walisema tunakimbia na ziada, na maji pia, kama ilivyosemwa na DAWASCO siku tatu zilizopita. Lakini leo, Jumapili, maji yamekata!

Abiria wapo, hivyo operesheni na mtaji wa matengenezo vipo.

Tatizo nini?

Wazalendo ndani ya TRC, tafadhali tujulishe kupitia njia zetu za kujuzana. Viongozi watatudanganya. Hawana dini. Waliwahi kusema Rais ametingwa na kazi Ikulu, kumbe ameshanyooka. Na waliongelea msikitini. Astakafullulilah Ladhim.

****
TAARIFA KUTOKA SHIRIKA LA RELI TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA
SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC) LINAOMBA RADHI KWA ABIRIA WA TRENI YA MCHONGOKO (EMU) WALIOANZA SAFARI YAO DAR ES SALAAM KWENDA DODOMA SAA 2:00 ASUBUHI NA KUSIMAMA GHAFLA MAJIRA YA SAA 2:20 KATI YA PUGU NA SOGA

AIDHA, TUNAOMBA RADHI PIA KWA ABIRIA WETU WA TRENI YA SAA 11:15 ALFAJIRI KUTOKA DODOMA NA TRENI YA SAA 3:30 KUTOKA DAR ES SALAAM IKIJUMUISHA SAFARI NYINGINE ZA SIKU YA LEO AMBAZO ZIMEATHIRIWA KUFUATIA HITILAFU KWENYE MIFUMO YETU YA UENDESHAJI

MAFUNDI WETU WAKO ENEO LA TUKIO WANAFANYIA ΚΑΖΙ CHANGAMOTO HIYO, TUTAENDELEA KUWAPATIA TAARIFA

TUNATANGULIZA SHUKURANI

View attachment 3142521
Chombo ni kipya, mitambo ya umeme ni mipya, na umeme upo. Nadhani juzi TANESCO walisema tunakimbia na ziada, na maji pia, kama ilivyosemwa na DAWASCO siku tatu zilizopita. Lakini leo, Jumapili, maji yamekata!😂
 
Mwanzo ni mgumu ndugu zangu! Tuwe wavumilivu kila kitu kitakaa sawa. Kumbukeni hatujwahi kuwa nazo treni hizi kabla.
Serikali isingekua na nia ya kuwasaidia wasafiri hasa katika upunguzaji wa ghalama, wasingejenga hii reli. Miundombinu yoyote inayojengwa hailengi kumkomoa mwananchi bali kumsaidia.
Ni vyema kutoa mawazo chanya kuliko kupopoa. Kumbukeni ni mali zetu wenyewe
 
Gentleman,
sasa ulitaka kifanyike nini zaidi ya matengenezo na marekebisho ya kiufundi ili hatimae safari iendelelee kwa usalama zaidi.

Lazima kua wastahimilivu, waangalifu na wenye subra sana kwenye masuala hususani ya usafiri wa kisasa unaotumia umeme 🐒
Marekebisho ya kiufundi ?

Kifaa kipya!

Ufundi wa nini ???

Niliishi Brooklyn, New York. Subway lao limejengwa mwaka wa 1904.

Sijawahi kuona limekata moto.

La kwetu lina miezi miwili unusu. Kila siku linakata moto porini.

Tatizo nini ????
 
Haya ndio madhara ya kufunga ndoa na mwanamke mwenye mtoto!

Madhara ya kujimilikisha Mali chakavu!
 
Binafsi sina lawama hata kidogo na SGR nasafiri kibos sana dar dom

Hayo ni makosa tu ya kibinadamu.
Mimi nasafairi sana na ndege lakini juzi dakika za mwisho nikaambiwa badala ya kuondoka mchana itakuwa jioni sababu ya kiufundi ni kweli unakuwa unakasirika kidogo lakini mwisho wa siku usalama na yanatokea haya lakini ukiuuliza % ngapi inatokea utakuta sio issue kabisa. Tuache kukuza mambo.
 
Mwanzo ni mgumu ndugu zangu! Tuwe wavumilivu kila kitu kitakaa sawa. Kumbukeni hatujwahi kuwa nazo treni hizi kabla.
Serikali isingekua na nia ya kuwasaidia wasafiri hasa katika upunguzaji wa ghalama, wasingejenga hii reli. Miundombinu yoyote inayojengwa hailengi kumkomoa mwananchi bali kumsaidia.
Ni vyema kutoa mawazo chanya kuliko kupopoa. Kumbukeni ni mali zetu wenyewe
= gharama

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Kama Boeing 737 max haina mwaka ilianguka Ethiopia,cha kushangaza nini,wanaojua maswala ya mechanics wanalijua hili,a machine is working to include an error.Vipi wale wanaokwenda kwenye anga za juu,chombo ni kipya na siku ya kulunch kinalipuka hewani!tuwe na subira kila kitu kitakaa sawa...
 
Gentleman,
sasa ulitaka kifanyike nini zaidi ya matengenezo na marekebisho ya kiufundi ili hatimae safari iendelelee kwa usalama zaidi.

Lazima kua wastahimilivu, waangalifu na wenye subra sana kwenye masuala hususani ya usafiri wa kisasa unaotumia umeme 🐒
Je, inashindikana Nini hilo treni kuvutwa na treni nyingine iliyo nzima ili iweze kufika stesheni na kuruhusu safari zingine za treni kuendelea na shughuli zake kwa mujibu wa ratiba zake? What's wrong about this?
Je, hao Watawala wa huko TRC wanahitaji kuwa na degree ngapi za chuo kikuu ili waweze kulitambua suala hili????
 
Hivi haya matreni yanavyobuma kila siku haiwezekani siku moja yakagongana?
Yani ilo swala nimeshajiuliza mara elf 1...maana inaonesha bado uendeshaji haujakaa sawa.
Hatuombei lakn inatia shaka ipo siku yataleta majanga
 
Imetoka Dodoma saa 12 kamili asubuhi.

Tangu saa mbili asubuhi, treni imekwama. Sasa inaenda saa 7 mchana, na hakuna matumaini ya kuendelea.

Treni iko kilomita 45 kutoka Dar, porini. Wengine wanashuka na kupanda boda; wanaenda wapi, sijui. Tangazo la TRC linasema mafundi wapo kazini.

Chombo ni kipya, mitambo ya umeme ni mipya, na umeme upo. Nadhani juzi TANESCO walisema tunakimbia na ziada, na maji pia, kama ilivyosemwa na DAWASCO siku tatu zilizopita. Lakini leo, Jumapili, maji yamekata!

Abiria wapo, hivyo operesheni na mtaji wa matengenezo vipo.

Tatizo nini?

Wazalendo ndani ya TRC, tafadhali tujulishe kupitia njia zetu za kujuzana. Viongozi watatudanganya. Hawana dini. Waliwahi kusema Rais ametingwa na kazi Ikulu, kumbe ameshanyooka. Na waliongelea msikitini. Astakafullulilah Ladhim.

****
TAARIFA KUTOKA SHIRIKA LA RELI TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA
SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC) LINAOMBA RADHI KWA ABIRIA WA TRENI YA MCHONGOKO (EMU) WALIOANZA SAFARI YAO DAR ES SALAAM KWENDA DODOMA SAA 2:00 ASUBUHI NA KUSIMAMA GHAFLA MAJIRA YA SAA 2:20 KATI YA PUGU NA SOGA

AIDHA, TUNAOMBA RADHI PIA KWA ABIRIA WETU WA TRENI YA SAA 11:15 ALFAJIRI KUTOKA DODOMA NA TRENI YA SAA 3:30 KUTOKA DAR ES SALAAM IKIJUMUISHA SAFARI NYINGINE ZA SIKU YA LEO AMBAZO ZIMEATHIRIWA KUFUATIA HITILAFU KWENYE MIFUMO YETU YA UENDESHAJI

MAFUNDI WETU WAKO ENEO LA TUKIO WANAFANYIA ΚΑΖΙ CHANGAMOTO HIYO, TUTAENDELEA KUWAPATIA TAARIFA

TUNATANGULIZA SHUKURANI

View attachment 3142521

Nimependa neno “Mchongoko”
 
Yani ilo swala nimeshajiuliza mara elf 1...maana inaonesha bado uendeshaji haujakaa sawa.
Hatuombei lakn inatia shaka ipo siku yataleta majanga
Naam.

Na mimi ni kama wewe. Siombei iwe hivyo, ila najiuliza tu kwa ufanisi huu mbaya, haiwezekani siku signal processing zikaharibika treni lisionekane kwenye system na lingine likaja kwa kasi likaligonga?

Hatuombei, tunafikiria tu.
 
Kama Boeing 737 max haina mwaka ilianguka Ethiopia,cha kushangaza nini,wanaojua maswala ya mechanics wanalijua hili,a machine is working to include an error.Vipi wale wanaokwenda kwenye anga za juu,chombo ni kipya na siku ya kulunch kinalipuka hewani!tuwe na subira kila kitu kitakaa sawa...
No, ndege ya Boeing 737 Max wakati ilipoanguka huko Ethiopia ilikuwa na umri wa zaidi ya mwaka mmoja, ndege hiyo ilinunuliwa mwaka 2017 na ilianguka mwaka 2019.
 
Back
Top Bottom