BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mabehewa 22 ya Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) yamedondoka mkoani Morogoro yakiwa na kemikali tani 1,099 za Sulphur Dioxide.
Wataalamu kutoka katika mamlaka mbalimbali za serikali wapo katika jitihada za kudhibiti madhara ya kemikali hizo kwa binadamu na wanyama baada ya treni hiyo kupata ajali katika eneo la Lumumwe, Halmashauri ya Mlimba wilayani Kilombero ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zambia.
Mkuu wa kitengo cha Usalama Shirika la Reli Tazara nchini Tanzania anayesimamia Kituo cha Mlimba Amani Mboliko amesema ajali hiyo imetokea baada ya hitilafu katika mfumo wa breki, na hivyo injini ilishindwa kuvuta behewa zote na kuifanya irudi nyuma kwa zaidi ya kilometa nane na kusababisha mabehewa yote kuanguka.
Meneja Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kati, Gerald Merinyo anasema tayari jitihada za kuhakikisha kemikali yote iliyomwagika inaondolewa zinaendelea kufanyika kupitia wataalamu mbalimbali.
HABARI LEO