Treni ya SGR kutoka Dar kwenda Dodoma yadaiwa kukwama tena baada ya Umeme kukatika Stesheni ya Kilosa

Umeme leo unasumbua,nilipo unakatika nakurudi
 
Wenye dhamana wanahujumu taifa.
Usafiri wa treni hii ni muhimu sana unatakiwa kypewa kipaumbele cha kipekee.
Mradi umekula mabilioni ya kutosha
 
Mapesa yaliyopotezwa kwa ajili ya kununua bling bling ya ndege ingewekezwa kwenye Solar power sasa hizi tungepunguza kero za umeme.
 
Ubabaishaji mwingi sana. Hivi ni kitu gani kinaweza kufanya kwa usahihi angalau 80% na serikali?
 
Kuwa na SGR ni hatua 1, kupitia changamoto zake na kupata uzoefu ni hatua ya 2, kuboresha na kusonga mbele ni hatua ya 3.

Kwa Taifa kama Tanzania nivema kujivunia kuwa na SGR kwani naamini miaka kadhaa ijayo tutapiga hatua zaidi mbali ya changamoto chache zinazotukumba.
 
Wa Tanzania gubu sasa unajuwa umeme umekatika shida nini? utasema kitu cha ajabu sana nchi nzima umeme umekatika sehemu kubwa kwa hiyo kusubiri tu imekuwa shida? Basi na siku zingine kukiwa hakuna shida zinafika salama muwe mnaandika sio negative tu.
Treni haitakiqi kukatika umeme, sawa na ndege haitakiwi kuisha mafuta, au hospitali umeme kukatika.
 
Kinachoongelewa ni tulivyodanganywa kuwa umeme ukikatika abiria hawatajua kwani treni haitasimama.
 
Hiyo treni inahudumia sehemu ndogo sana ya watanzania hata humo ipitamo, ukipanda Dar inasimama Ngerengere na Morogoro, wengine wote njiani wanaiona kama muvi tu, sijui hayo nayo ni mafanikio!
 
Hiyo treni inahudumia sehemu ndogo sana ya watanzania hata humo ipitamo, ukipanda Dar inasimama Ngerengere na Morogoro, wengine wote njiani wanaiona kama muvi tu, sijui hayo nayo ni mafanikio!
Kaka hizi zote ni hatua tuko ya kwanza tunaelekea ya pili tutafika ya tatu.

Bora kitu kuliko kukosa kitu, sisi tuishi na tutoe mawazo yetu sehemu husika ipo siku tutakuwa kama wale, tujipe muda kwani ni mwalimu sahihi.

Kwangu ni mafanikio kwani tumetoka 0 tupo 1, hope tutafika 3.
 
Sgr imekuja tanzania kwa wakati mzuri lakini ilibidi ijitasmini kabla ya mchakato wa treni ya mwendo kasi kunza kujua tatizo la upatikanaji umeme na vya nzo vyake vyote vya upatikanaji wa umeme kwa nchi za wenzetu zilizo endelea siku kama ya leo unakuta umesha poteza ma bilioni ya pesa kwa sababu ya umeme au usafiri shaji kwa njia ya treni ya sgr ushauri wangu kwa nini tusi we na mbinu nyingine ya badae kwa ajiri ya kuokoa tatizo ili la ukati kaji wa umeme. Moja kuna njia nyingi sana za upatikani wa umeme na ikatumik kwa ajiri ya uduma flani kama iyo ya sgr 1. Kuna umeme wa jua sola sasa ivi umeme wajua una uwezo mkubwa wakuendesha mitambo mikubwa katika teknologia yetu ya sasa tulikuwa tuna uwezo wa kuwekeza uko tuna maeneo mengi ya wazi kwa ajiri ya kupata nishati jua ya kiwango cha juu zaidi na tukaendesha mitambo yetu vizuri zaidi.

2. Tuna usawa wa bahari mzuri kabisa pia tulikuwa na uwezo wa ku pata umeme wetu kwa njia ya mashine za kata upepo na tuka zarisha umeme wa kutosha kuwezesha nchi ikawa na uzarishaji mwingi wa umeme wakutosha tuna nyika nyingi zenye upepo mzuri na mkari wenye kuweza kuendesha iiizi mashine tuna bahari na maeneo ya bahari mazuri lkn tunashindwa kuyatumia ipasavyo na kuwa na mawazo chanya ya kujifunza kwa wenzetu walio tuvuka kinishati.

Itimisho langu ni..

Ivi vyanzo ni vizuri sana kwqmba vinge saidia kwa atua ya hawari mfano kama kungekuwa na switch kama umeme wa tanesco umekatika auto matiki leo tunakonecti umeme wetu kwenye njia ya sola au umeme kata upepo na uduma zingine zikiendelea na serikari kupata kipato kupitia iizi uduma mizigo inge fika kwa wakati sehemu usika...Ushauri tufike wakati tubadilike na mifumo yetu ya umeme zipo njia nzuri lakn tuna shindwa kuzitumia mungu ametupa nishati ya jua lakn tunashindwa kuzitumia.

Na ya mwisho pia umeme uu ungekuwa ngao kwenye vituo vya afya pia kungeokoa garama ya matumizi ya unit za umeme wa tanesco unauwezo wa mchana ukatumia nguvu ya sola bila kuisha chaji na usiku ukatumia umeme wa tanesco.
 
Wewe hapo mtaani dukani kwa mangi unalipa VAT? unapata risiti ina Vat? hayo unayaona ukienda kwenye sehemu kama shoppers unaona VAT kiasi gani umelipa niambia mtaani kwako unapewa risiti kwa Mangi?
 
Umeandika Kiswahili au kinywaranda?
 
Kama wewe kulipa VAT umejiona ndio mlipa kodi na kupiga kelele basi kuna watu wanalipa kila mwezi kanunua bidhaa hajanunua wanalipa. Wewe una hiyari unalipa kwa mujibu wa mahitaji yako ndio maana nchi zingine ukinunua kitu kama mgeni ukitoka unarudishiwa VAT uliyolipa.
 
Hamna shukrani hata kidogo,binadamu aliyezitrengeneza anaugua sembuse treni
 
Ni kweli umeme ulikatika, hadi huku Kahama haukwepo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…