Treni ya SGR kutoka Dar kwenda Dodoma yadaiwa kukwama tena baada ya Umeme kukatika Stesheni ya Kilosa

Bora kusema kweli hautasutwa kesho kuliko kudanganya ili usisiwe kwani kesho utasutwa, lakini unapoanza anza na kipya kuliko kuanza na mitumba wakati pesa ya kununua kipya unazo.
 
Ndege gani uliambiwa mafuta yakikata itaendelea kuruka! Tusipende kuambiwa uongo na tukafurahia kudanganywa.
 
Wa Tanzania gubu sasa unajuwa umeme umekatika shida nini? utasema kitu cha ajabu sana nchi nzima umeme umekatika sehemu kubwa kwa hiyo kusubiri tu imekuwa shida? Basi na siku zingine kukiwa hakuna shida zinafika salama muwe mnaandika sio negative tu.
Wamezoea sana yaan siku hizi waandishi wengi humu mitandaoni utakuta mtu anaandika kitu hata hajashuhudia
 
Ndege gani uliambiwa mafuta yakikata itaendelea kuruka! Tusipende kuambiwa uongo na tukafurahia kudanganywa.
Wapi nimeandika ndege haina mafuta? nimekwambia hata ndege zinachelewa kwa sababu zake za kindege na tunakubali delays wakati mwingine wala sio sababu za msingi unaambiwa tu sababu za kiufundi, sasa cha ajabu nini delay ya Train tena tunajuwa sababu ni nini? acheni hizo porojo zenu. Train inasafirisha maelfu ya watu daily salama hamuoni ila hitilafi zikotokea mnajitokeza.
 
Wamezoea sana yaan siku hizi waandishi wengi humu mitandaoni utakuta mtu anaandika kitu hata hajashuhudia
Wako watu na chuki tu hawatakii mema nchi hii, kosoa ili kuboresha na uhakika kuna watu na hiyo SGR wamefika kabla hata yule aliyetoka Gongo la Mboto kwenda Mbezi.
 
Wako watu na chuki tu hawatakii mema nchi hii, kosoa ili kuboresha na uhakika kuna watu na hiyo SGR wamefika kabla hata yule aliyetoka Gongo la Mboto kwenda Mbezi.
Yaan wanaombea leo kesho SGR ife mi nazan hawa ni makondakta wa mabasi yale yanayoelekea SGR inapita kwahyo ugali wao unapungua
 
BUNDI,NYANI NA FISI WAKAMATWE HARAKA.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa, amesema wananchi waondoe hofu "kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme katika safari za treni inayotumia umeme akisema treni hiyo ina mkondo wa umeme unaojitegemea.Hayo yamesemwa Februari 26, 2024".
 
Nadhani tunamjadili mtu sasa sio issue, ok nakubaliana yeye mkurugenzi anajadiliwa kwa kauli zake ni wajibu wake kutoa ufafanuzi kama yeye.
 
Zingetakiwa ziwe zina alternative Batteries sasa wakubwa wakatuambia zinatumia diesel duuh
 
Treni ya SGR iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma imelazimika kusimama kwenye Stesheni ya Kilosa baada ya Umeme kukatika, abiria wanasubiri umeme urudi ndio safari iendelee, wameambiwa Grid ya Taifa imezima.
 
Tanzania eeee
Tanzania eeee
Tanzania eeee
🀣🀣🀣🀣🀣
 
Bora kusema kweli hautasutwa kesho kuliko kudanganya ili usisiwe kwani kesho utasutwa, lakini unapoanza anza na kipya kuliko kuanza na mitumba wakati pesa ya kununua kipya unazo.
Kaka tusiwalaumu hao wenye nafasi kwa sasa, najua kukosoa ni kazi rahisi sana lakini ngumu nikuwa katika hiyo nafasi.

Hii kitu ilinisumbua sana zamani kwanini watu hawawi wakweli kwa kila kitu hadi mwaka 2021 niliposoma kitabu cha Dale Carnegie kinachoitwa "how to win friends and influence people"

Alisema "katika communication always ongea mambo ambayo wasikilizaji wanatamani kusikia na sio uharisia" haya nimeyaona kwenye mazingira tofauti sana
Mfano, 1. ukienda kukopa unaenda na tarehe ya kurudisha hata kabla ya kuulizwa ili mkopaji aone nia njema yako hata kama umepanga kudhurumu
2. Kama unafamilia always utaongea vitu positive kwa watoto hata kama khali yako ya kiuchumi ni duni (huwez wambia tutakufa wanangu but you go for the hope)
3. Mwanasiasa hawezi ongea uharisia wakati unaowambia ndio watoa pesa na bado hawajakupa so lazima aongee kitu ambacho wasikilizaji watafurahia

What fact n kwamba usichukulie kila kauli katika siasa kuwa itakuja kama ilivyosemwa wanaishi katika mazingira ya forecast the future na prediction na ndio maana mwanasiasa mzuri huoaswa kuwa interchangeable.

Thank you
 
Sisi tunaotumia grid yenye chanzo cha RUSUMO-NGARA,yaani Kigoma,Kagera,Geita umeme upo vizuri tu.
 
Imekuaje tena huko, inamaana huyu jamaa alidanganya umma πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€, ingekuwa kwa wenzetu alipaswa kuwajibika kwa kauli hii lakini kwasababu tupo kwenye shamba la Bibi tunasema tu inshallah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…