Treni ya SGR kutoka Dar kwenda Dodoma yadaiwa kukwama tena baada ya Umeme kukatika Stesheni ya Kilosa

Treni ya SGR kutoka Dar kwenda Dodoma yadaiwa kukwama tena baada ya Umeme kukatika Stesheni ya Kilosa

Kaka hizi zote ni hatua tuko ya kwanza tunaelekea ya pili tutafika ya tatu.

Bora kitu kuliko kukosa kitu, sisi tuishi na tutoe mawazo yetu sehemu husika ipo siku tutakuwa kama wale, tujipe muda kwani ni mwalimu sahihi.

Kwangu ni mafanikio kwani tumetoka 0 tupo 1, hope tutafika 3.
Bora kusema kweli hautasutwa kesho kuliko kudanganya ili usisiwe kwani kesho utasutwa, lakini unapoanza anza na kipya kuliko kuanza na mitumba wakati pesa ya kununua kipya unazo.
 
Uzuri nchi hii kuna option nyingi sana, kuna ndege, ma bus na SGR ni mtu kuamua tu hapa nimepigwa napanda huku lakini leo hii unaweza kwenda kukata ticket full train 4 daily zaidi ya watu alfu 3 wanaingia na kutoka ukiangalia data ni mafanikio kuliko hizi changamoto. Hata ndege huwa zinachelewa sana tu lakini watu wanakubali ni changamoto
Ndege gani uliambiwa mafuta yakikata itaendelea kuruka! Tusipende kuambiwa uongo na tukafurahia kudanganywa.
 
Wa Tanzania gubu sasa unajuwa umeme umekatika shida nini? utasema kitu cha ajabu sana nchi nzima umeme umekatika sehemu kubwa kwa hiyo kusubiri tu imekuwa shida? Basi na siku zingine kukiwa hakuna shida zinafika salama muwe mnaandika sio negative tu.
Wamezoea sana yaan siku hizi waandishi wengi humu mitandaoni utakuta mtu anaandika kitu hata hajashuhudia
 
Ndege gani uliambiwa mafuta yakikata itaendelea kuruka! Tusipende kuambiwa uongo na tukafurahia kudanganywa.
Wapi nimeandika ndege haina mafuta? nimekwambia hata ndege zinachelewa kwa sababu zake za kindege na tunakubali delays wakati mwingine wala sio sababu za msingi unaambiwa tu sababu za kiufundi, sasa cha ajabu nini delay ya Train tena tunajuwa sababu ni nini? acheni hizo porojo zenu. Train inasafirisha maelfu ya watu daily salama hamuoni ila hitilafi zikotokea mnajitokeza.
 
Wamezoea sana yaan siku hizi waandishi wengi humu mitandaoni utakuta mtu anaandika kitu hata hajashuhudia
Wako watu na chuki tu hawatakii mema nchi hii, kosoa ili kuboresha na uhakika kuna watu na hiyo SGR wamefika kabla hata yule aliyetoka Gongo la Mboto kwenda Mbezi.
 
Wako watu na chuki tu hawatakii mema nchi hii, kosoa ili kuboresha na uhakika kuna watu na hiyo SGR wamefika kabla hata yule aliyetoka Gongo la Mboto kwenda Mbezi.
Yaan wanaombea leo kesho SGR ife mi nazan hawa ni makondakta wa mabasi yale yanayoelekea SGR inapita kwahyo ugali wao unapungua
 
Treni ya SGR iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma imekwama kwenye Stesheni ya Kilosa baada ya Umeme kukatika, tuko hapa tunasubiri umeme urudi ndio safari iendelee, tumeambiwa Grid ya Taifa imezima.."

Kabla hayajafika tulishauri haya Madude yaje na "Power bank" lakini Mfumgwa wetu mtarajiwa Bwana Kadogosa akasema umeme ukikatika yanatumia Diesel.

Haya Kiko wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....?

Pia soma ~ TRC: Treni za SGR zilisimama maeneo matatu tofauti kutokana na hitilafu ya umeme katika Gridi ya Taifa
BUNDI,NYANI NA FISI WAKAMATWE HARAKA.
 
Wapi nimeandika ndege haina mafuta? nimekwambia hata ndege zinachelewa kwa sababu zake za kindege na tunakubali delays wakati mwingine wala sio sababu za msingi unaambiwa tu sababu za kiufundi, sasa cha ajabu nini delay ya Train tena tunajuwa sababu ni nini? acheni hizo porojo zenu. Train inasafirisha maelfu ya watu daily salama hamuoni ila hitilafi zikotokea mnajitokeza.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa, amesema wananchi waondoe hofu "kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme katika safari za treni inayotumia umeme akisema treni hiyo ina mkondo wa umeme unaojitegemea.Hayo yamesemwa Februari 26, 2024".
 
Nadhani tunamjadili mtu sasa sio issue, ok nakubaliana yeye mkurugenzi anajadiliwa kwa kauli zake ni wajibu wake kutoa ufafanuzi kama yeye.
 
Zingetakiwa ziwe zina alternative Batteries sasa wakubwa wakatuambia zinatumia diesel duuh
 
Treni ya SGR iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma imelazimika kusimama kwenye Stesheni ya Kilosa baada ya Umeme kukatika,
1733315682043.jpg
abiria wanasubiri umeme urudi ndio safari iendelee, wameambiwa Grid ya Taifa imezima.
 
Bora kusema kweli hautasutwa kesho kuliko kudanganya ili usisiwe kwani kesho utasutwa, lakini unapoanza anza na kipya kuliko kuanza na mitumba wakati pesa ya kununua kipya unazo.
Kaka tusiwalaumu hao wenye nafasi kwa sasa, najua kukosoa ni kazi rahisi sana lakini ngumu nikuwa katika hiyo nafasi.

Hii kitu ilinisumbua sana zamani kwanini watu hawawi wakweli kwa kila kitu hadi mwaka 2021 niliposoma kitabu cha Dale Carnegie kinachoitwa "how to win friends and influence people"

Alisema "katika communication always ongea mambo ambayo wasikilizaji wanatamani kusikia na sio uharisia" haya nimeyaona kwenye mazingira tofauti sana
Mfano, 1. ukienda kukopa unaenda na tarehe ya kurudisha hata kabla ya kuulizwa ili mkopaji aone nia njema yako hata kama umepanga kudhurumu
2. Kama unafamilia always utaongea vitu positive kwa watoto hata kama khali yako ya kiuchumi ni duni (huwez wambia tutakufa wanangu but you go for the hope)
3. Mwanasiasa hawezi ongea uharisia wakati unaowambia ndio watoa pesa na bado hawajakupa so lazima aongee kitu ambacho wasikilizaji watafurahia

What fact n kwamba usichukulie kila kauli katika siasa kuwa itakuja kama ilivyosemwa wanaishi katika mazingira ya forecast the future na prediction na ndio maana mwanasiasa mzuri huoaswa kuwa interchangeable.

Thank you
 
Sisi tunaotumia grid yenye chanzo cha RUSUMO-NGARA,yaani Kigoma,Kagera,Geita umeme upo vizuri tu.
 
Imekuaje tena huko, inamaana huyu jamaa alidanganya umma 😀😀😀, ingekuwa kwa wenzetu alipaswa kuwajibika kwa kauli hii lakini kwasababu tupo kwenye shamba la Bibi tunasema tu inshallah
Screenshot_20241204-172914.png
 
Back
Top Bottom